Fatilia andiko hili..
Ayubu 22:12 “Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!
13 Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?
14 Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU.
15 Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu “;
Kuba ni mzunguko wa anga, unapoangalia juu angani utagundua kuwa ncha za mbingu zinaonekana katika umbo la duara ndio maana jua lipochomoza asubuhi huwa linaonekana likitokea chini upande wa mashariki na wakati wa mchana huonekana likiwa katikati na kisha huzama chini upande wa magharibi…
Huo mduara unaonekana angani hujulikana kama ‘Kuba`
Biblia inatuambia Mungu anatembea juu ya huo mduara ili autangaze utukufu wake kila mtu auone..
Ayubu 22:14 “Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU”.
Andiko hili linatupa ujumbe kuwa Mungu ni mkuu sana na yupo juu ya vyote tena uwezo wake ni mkubwa.
Je upo kwake yeye aliyeumba vyote vilivyo mbinguni na duniani? Kama bado basi leo rudi kwake kabla neema yake haijaisha
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua,..
Maran atha …
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.