FAHAMU MAPEPO YANAVUTIWA NA NINI KWA MWAMINI?
Shalom nakusalimu katika jina la mwokozi wetu karibu tuyatafari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.
Umeshawahi kufikiri ni kwa nini Wakristo wengi wanafanyiwa ukombozi(deliverance) kutoka kwenye vifungo vya adui ilihali hapo awali walikua wameokoka? Hebu tutafakari mstari huu Bwana Yesu anamwambia mwanamke mmoja aliekuwa amekamatwa kwenye uzinzi na mafarisayo wakamleta kwake ili kumjaribu.
Yohana 8:11 “Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]”
Kwa nini Bwana Yesu alimsisitiza kwamba asitende dhambi tena? Sasa ili tuelewe vizuri
Mathayo 12:43-45 “ Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.
[44 ]Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.
[45 ]Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.”
Unaona hapo anasema “Pepo mchafu…..”
Maana yake hayana sifa ya usafi na hayawezi kukaa sehemu safii hata siku moja…
Mapepo yanavutiwa sana na uchafu ni kama nzi, nzi wanavutiwa na sehemu yoyote iliyo chafu, mahali popote palipo na uchafu utakuta nzi wapo wengi sana, nilipokua katika tafakari Bwana akanipa mfano mwingine akaniambia…” ni sawa sawa na nzi kwenye kidonga wanavutiwa sana kukaa pale hata kama ukiwafukuza madam bado kidonda kipo watarudi tena na tena suruhisho sio kuwaua wale nzi suruhisho ni kutibu kile kidonda kikipona wale nzi huwezi ukawaona tena wakitua mahali pale ikiwa palikua ni mguuni au mkononi au sehemu yoyote huwezi kuwaona tena.”
Mungu akaniambia kama huo mfano huo ulivyo na ndio ilivyo kwa mtu ambae ameokoka lakini maisha yake yana uchafu(Spiritual garbage) yaani uchafu wa kiroho huyo mtu mapepo yatamsumbua mara kwa mara na hata kama ataombewa ataomba yeye ila kama hajaamua au kuchukua jukumu la kutibu hicho kidonda yaani uchafu wa kiroho kuuondoa atakaa katika hali ya mateso(demonic visitation)siku zote kwa sababu mapepo kitu yanachovutiwa nacho ni uchafu, hivyo suruhisho sio kuomba sana na kuwekewa mikono nk suruhisho ni kuhakikisha yeye mwenyewe anaondoa hicho kitu kinachovutia mapepo uchafu(garbage).
Hivyo Mlang wowote ukiwa uko wazi mapepo yanatumia mlango huo huo tu kuingia ndani na kupitia mlango huo yanakwenda kuzalisha vitu viovu zaidi ndani yake kwa sababu ikiwa yamefanikiwa kuweka makao tegemea yataanza kuweka vitu vingi yanavyoendana navyo. Ni sawa na wewe unavyohamia kwenye nyumba mpya kuna namna wewe utataka iwe na muonekano Fulani ndani utapanga vitu tofauti na yule aliekuwemo ndicho mapepo yanachokifanya.
Utakuta mtu alikua natabia za kuangalia picha Instagram tu za watu waliovaa vibaya atatoka hapo ataanza kutamani kuangalia picha za uchi kabisa, taratibu anafikia katika hali ya kuanza kujichua, anafikia katika hatua ya kuzini kabisa.
labda ilikua ni swala la hasira linamsumbua ataanza kukasirika pale anapoudhiwa hata kidogo na kuweka visasi ndani yake(asiachilie/kusamehe) taratibu hiyo hasira itakua atafikia hatua ya kupasua vitu, na mwisho kupiga ikiwa ni mke au mtoto na anaweza akajikuta anaua na anakuja kuelewa amefanya upumbavu baada ya kufanya hilo jambo. Kwa sababu yuko under demonic influence/power bila kujua..
Vivyo hivyo ikiwa ni wizi,useng’enyaji nk pale hivi vitu vinapoendelea kuwa ndani yake.
Sasa jambo ambalo linaweza kukusaidia/kumsaidia ni kuanza ku deal na hizo tabia kujidhibiti huku akitafuta msaada wa kimaombi yeye aanze kufanya hima ya kufunga milango hiyo ndani yake. Watu wengi wana focus na tatizo baada yaku focus na chanzo cha tatizo kwa sababu ukishadhibiti chanzo hakuna tatizo linaweza kutokea.
Kuna kitu kinaitwa katika ulimwengu wa roho Spiritual legality maana yake uhalali wa kiroho/ haki ya kisheria maana yake unapokubali kuendelea kukaa katika hali hiyo kwa muda hiyo legality shateni anakua nayo kwa sababu umeshikiria au una kitu chake.
Mambo ya mwilini hapa ni kivuli cha uhalisia uliopo rohoni mfano wewe ni raia mwema na huru lakini ukifanya kosa unageuka kuwa mharifu maana yake unawapa uhalali police kukukamata, utetezi wa mahakama utakuwepo unaweza ukaendesha kesi hueda ukashida na rohoni iko hivyo tunapokosea tunampa uhalli shetani wa kutushitaki damu ya Yesu ipo kututetea lakini haiwezi kutetea kwa mtu ambae anafanya makosa kwa kukusudia ndivyo hivyo huku mwilini ukikamatwa na kosa ambalo ulikusudia ukalifanya unakua katika hali mbaya hata kama utaendesha kesi kwa pesa nyingi itafikia hatua ukweli utadhirika na utafuungwa.
Hivyo shughulika na chanzo zaidi..
Kwa sababu kukiwa hakuna chanzo tatizo haliwezi kuwepo.
Na mtu anawezaje kudhibiti akawa salama? Ni yeye kuwa na moyo wa kukusudia kubadilika ndani yake, kusoma neno la Mungu na kuwa mtu wa maombi na kutafuta msaada kwa watumishi wa Mungu na Bwana atawatumia kumsaidia na kuwa salama. Shetani siku zote anavutiwa na uchafu ndio maana anatutia uchafu hata kupitia ndoto kusudi apate mlango tu.
Kwa jina la Yesu Kristo haitakua kwako..
Nimekuombea neema ya Bwana Yesu ikusaidie uweze kusimama imara na kushinda na kuwasaidia wengine zaidi. Shetani hatakua na mamlaka juu yako Fanya bidii kuondoa uchafu wala shetani hatasogea maana hapendi kitu kinachoitwa usafi.
@Nuru ya upendo.
Phone contacts: 0613079530
For spiritual counseling and spiritual growth and transformation.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.