Fahamu tofauti kati ya maovu na maasi

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom

JE ipo tofauti Gani kati ya ‘Maasi’ na ‘Maovu’?

Maovu ni yale mambo afanyayo mtu kinyume na Maagizo ya Mungu, nayo hutokana na Shetani (Mwovu, mathayo 5:37) mfano wa Maovu ni Uasherati, Ulawiti, Ufiraji, dhuluma, ibada za sanamu na yote yanayofanana na hayo.

Maasi ni yale Maovu yanayofanywa na Watu waliomjua Mungu Kisha wakajitenga na imani, kwa lugha nyingine huitwa Ukengeufu, kurudi Nyuma au anguko la mwamini!

Mtu wa kidunia hawezi kufanya maasi! yeye anafanya Maovu, Maana maasi yanafanywa na walioasi Imani. Yani mtu alikuwa mwongofu au anayemjua Mungu na kuyafanya mapenzi ya Mungu, halafu baadae anarudi tena kufanya yale Maovu aliyokuwa akiyafanya kabla, hapo ndipo anafanya Maasi! Ambayo hukumu yake ni kubwa kuliko Maovu, kama tunavyosoma katika injili ya Luka..

Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.

48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na Zaidi”.

Mfano wa Watu waliokuwa wakifanya Maovu ni Sodoma na Gomora..

Mwanzo 19:15 “Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika MAOVU YA MJI HUU.”

Na mfano mzuri kwa waasi ni wana wa Israel..

Yeremia 3:21-22
“21 Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau Bwana, Mungu wao.

22 RUDINI, ENYI WATOTO WAASI, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u Bwana, Mungu wetu.”

Maandiko yanasema Siku za Mwisho maasi yataongezeka zaidi! Yaani wale Waamini wanaorudi nyuma kuwa wengi kuliko hata Waovu au watu wa kidunia

Mathayo 24:12 “Na kwa sababu ya KUONGEZEKA MAASI, upendo wa wengi utapoa”.

Ukifanya Udanganyifu, Uongo, Uasherati, Ibada za sanamu, Utoaji mimba, wizi angali unamjua Kristo yaani Umeokoka unafanya Uasi. Ambayo hiyo roho ya kuasi hutokana na MPINGA-KRISTO (2 Thethalonike 2:7)

Wapendwa pamoja na kuwa hajadhihirishwa bado MPINGA-KRISTO lakini huenda roho yake inafanya kazi tayari ndani ya makanisa. Bwana Atusaidie tudumu katika kweli yake tusiangukie Maasi.

Ikiwa bado unaishi ukifanya Maovu jua hatma ya Waovu wote ni katika lile ZIWA la moto, hivyo ni heri Ukabidhishe maisha yako kwake Yesu Kristo akusafishe na upate Uzima wa milele.

Amen

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *