Nini maana ya apataye mke apata kitu chema ?

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tujifunze Maneno ya Uzima.

Swali: Je! Mtu aliyeoa hujiongezea kibali zaidi mbele za Mungu kuliko ambaye bado hajaoa?! Kulingana na Andiko hili..

Mithali 18:22

Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.

Jibu: La! Si kweli kwamba kuoa ni kujiongezea kibali mbele za Mungu. Kibali mbele za Mungu hupatikana kwa njia moja tu! Nayo ni “kuyafanya yaliyo mapenzi ya Mungu”

Kama alivyomwambia kaini maneno haya..

Mwanzo 4:7

[7]”Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. “

Pia Maandiko yanasema asiyeoa au kuoelwa anayo nafasi kubwa Zaidi kumtumikia na kumpendeza Mungu kuliko aliyeoa au kuoelwa..

1 Wakorintho 7:32-33

[32]”Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

[33]bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe. “

Sasa turejee ” Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA”.

Ni kibali Gani?

Kwanza kabisa ni kwamba Mungu hubariki ndoa, pia ni jambo jema mbele zake. Hivyo aingiae katika ndoa Hatapunguza ukaribu na Mungu Wala hatojiongezea nafasi ya kumkosea, na kinyume chake awe na furaha katika hiyo, na atapata kibali tu.

Faida zinazoambatana na ndoa ni kama vile Heshima katika Jamii, kuepuka Zinaa, kuongeza Uaminifu wa mtu na zaidi ni jambo jema katika Huduma na Utumishi wa Kiroho.

Ndoa Haina nafasi ya kuongeza kibali zaidi mbele za Mungu, Kuliko ambao hawajaoa. Tunajifunza kwa habari ya Mtume Paulo, Barnaba, pamoja na Mwokozi wetu Yesu Kristo kuwa hawakuoa lakini walikuwa karibu zaidi na Mungu.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *