Hapana hekima wala ufahamu wala shauri juu ya Bwana

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom.

Swali: Nini maana ya hakuna hekima Wala Ufahamu Wala shauri juu ya Bwana?

Mithali 21:30

30 Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.

Jibu: tunaweza kulielezea kwa wepesi zaidi kama ” hakuna hekima Wala Uelewa/ufahamu au Shauri la kibinadamu linaloweza kusimama kinyume na Mungu”. Kama Maandiko yanavyosema katika Wakorintho

1 Wakorintho 3:19
19 “Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.”

Mungu ndiye mwenyezi, Mkuu wa yote Muumba wa mbingu na nchi! Ni nani [binadamu] awezaye kufanya jambo lolote kinyume na Agizo lake likafanikiwa? Jibu ni Hakuna!
Hata Juhudi za shetani kuharibu kanisa la Mungu halitaweza kufanikiwa hata angalifanya Juhudi kiasi Gani.

Hakuna jambo linalotokea ghafla kwake [Surprise] Kama kwetu sisi wanadamu. Wanasayansi wanakataa uwepo wake kwa hekima zao Wakisema “Binadamu alitokana na nyani”! Lakini watarudi kule kule katika Uumbaji, maarifa [sayansi na teknolojia] yanaongezeka vizazi na vizazi lakini yeye atabaki kusimama kama Mungu!

Mwanadamu hawezi kuukimbia USO wa Mungu popote, yeye ndiye ayajuaye mawazo na Nia za mioyo yetu tokea mbali hatuwezi kumficha jambo lolote kwa hekima zetu [zilizotokana na yeye].

Tusome..

Zaburi 50:17″ Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. 18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.

19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila. 20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.

21 NDIVYO ULIVYOFANYA, NAMI NIKANYAMAZA; UKADHANI YA KUWA MIMI NI KAMA WEWE. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.

22 Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane mwenye kuwaponya.”

Chanzo kikubwa Cha kutomhofu Mungu ni kudhani yeye ni Kama sisi. Mfano watu wamekuwa na Udhuru nyingi katika kuifanya kazi ya Mungu, mtu anasingizia anakosa muda wa kusoma biblia, kufanya maombi na huduma nyinginezo kwa kisingizio Cha kuchoka bila kujua ya kuwa Mungu anawajua vyema nia zao, na atawaonesha waliochoka zaidi yao na hawana hizo Udhuru.

Yote ni kwa sababu hakuna hekima Wala shauri linalosimama kinyume na Mungu.

Amen

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *