Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Tofauti kati ya kuwa Mtakatifu (1petro 1:15-16) na kuwa mkamilifu (Mathayo 5:48)
MTAKATIFU ni mtu msafi, aliyetakaswa, afanyaye matendo mema na asiye na mawaa. Biblia inatuasa tuwe watakatifu kama alivyo Baba yetu wa Mbinguni
1Petro 1:15 “bali kama yeye aliyewaita ALIVYO MTAKATIFU, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU”.
Utalikuta Agizo hili ata katika torati
Walawi 19:2 “Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu”.
Lakini MKAMILIFU ni mtakatifu kamili, maana wapo watakatifu wasiokuwa Wakamilifu. Mtakatifu aliyekamilika utamtambua kwa jambo la ziada linalomtofautisha na watakatifu wengine!
Mambo kama yaliyoagizwa na Masihi wetu Yesu Kristo..
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, MNATENDA TENDO GANI LA ZIADA? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
48 Basi ninyi MTAKUWA WAKAMILIFU, KAMA BABA YENU WA MBINGUNI ALIVYO MKAMILIFU”
Ni jukumu la kila Mwamini kutafuta kuwa mkamilifu na si kuishia kuwa Mtakatifu pekee.
>>Kufunga na kuomba: mtakatifu anafunga na kuomba kwa ajili yake Lakini mkamilifu hufanya kwa faida ya wengine pia
>>Mtakatifu husoma Biblia na kuomba, lakini Mkamilifu husoma neno, kuomba na kufundisha wengine juu ya Yale anayojifunza.
>>Mtakatifu hufanya kazi ya Mungu kwa Moyo Ili apate thawabu Mbinguni lakini Mkamilifu hawazi thawabu zake pekee katika kufanya kazi ya Mungu Bali hufikiri pia kuhusu ndugu zake wasipotee na kuangamia katika adhabu ya Mungu ya milele.
>>Mtakatifu hukusanyika siku moja pekee katika wiki kukusanyika, lakini ni zaidi kwa Mkamilifu.
>> Mtakatifu huzishika Amri za Mungu lakini moyo wake huwa katika Mali pia tofauti kabisa na mawazo ya mkamilifu. Tuangalie mfano huu..
Mathayo 19:16 “Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?
17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo,
19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
20 Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena?
21 Yesu akamwambia, UKITAKA KUWA MKAMILIFU, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi”.
Nuhu alikuwa mkamilifu katika vizazi vyake naye akaponywa na gharika (Mwanzo 6:9), Daudi alikuwa mkamilifu hata akawa rafiki wa Mungu (2 Samweli 22:24), Ayubu kwa Ukamilifu wake akamwona Mungu katikati ya majaribu (Ayubu 1:1)
Mungu wetu ni mwaminifu, tutakapokuwa wakamilifu tutamwona wakati wa Majaribu.
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.