Je kuna dhambi kubwa na ndogo?

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Swali: JE dhambi zote ni sawa? Hakuna iliyo kubwa na ndogo? Yaani aliyeua na anayesengenya au kusema Uongo ni sawa?

Jibu: turejee Maandiko yanasema Nini kuhusu Hilo

Yakobo 2:10 “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. “

Hivyo basi, dhambi zote ni sawa hakuna iliyo kubwa Wala iliyo ndogo, zote mwisho wake ni adhabu ya Mungu!
Japo zinatofautiana kutokana na mtu husika, kwa mfano zaidi turejee Maandiko haya

Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, ATAPIGWA SANA.

48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, ATAPIGWA KIDOGO. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi. “

Adhabu zinatofautiana kulingana na taabu ya mtu husika juu ya Kristo, kipindi alichoishi duniani, kadhalika hata na jehanum hulingana pia jinsi mtu alivyopuuza Neema ya wokovu.

Yote katika Yote hauruhusiwi kupima dhambi zozote Bali kuziepuka, maana zimebeba ghadhabu Kali ya Mungu juu yake, na mshahara wa dhambi [iwe kubwa au ndogo] ni mauti. (Warumi 6:23)

Kama bado hujampa Yesu Kristo maisha yako njoo Sasa! Uone pendo lake la ajabu, ujue ya kuwa anakupenda pamoja na dhambi zako na alikufia pale Msalabani! Tubu Leo na umgeukie yeye upate Uzima wa milele.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *