Shalom.
Kwanza tujue ya kwamba Ahadi za Mungu wetu zinaonekana katika matatizo au shida zetu. Hivyo shida zetu ameziruhusu ili tumwone yeye kwa vitendo, mfano tungeutafutaje wokovu angali hakuna dhambi?, tungejuaje ni mponyaji bila kuugua, tungejuaje Wingi wa Rehema zake bila kuanguka dhambini, tungejuaje haki yake bila sisi wenyewe kutokuwa na haki? Na mengine mengi kama hayo..
Majaribu ni mtaji au nyenzo pekee ya Kuongeza imani zetu, hata dhahabu ni sharti ipitishwe katika moto ili ing’ae maradufu. Na hiyo ndio sababu ya Shetani[Nyoka/joka] kuwepo hata Leo angali Mungu alikuwa anao uwezo wa kumuondoa tangu pale Edeni. Hata Tulipokuwa shule walimu walitunga mitihani yenye maswali Magumu na mitego mingi si ili tufeli, bali tuimarike zaidi kimaarifa! Sasa ni hivo hata kwa Mungu wetu ambae yeye hutuwazia yaliyo mema..
Yeremia 29:11 ” Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”
Zaburi 103:12-15
12″ Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.
14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.
15 Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.”
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.