Farao alikufa yeye pamoja na jeshi lake?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu asifiwe, Karibu katika kujifunza

Vifungu  hivi vitatusaidia kujua  jibu kulingana  na swali hapo juu

Kutoka 14:28

[28]Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.

Tusome tena

Kutoka 15:19

[19]Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.

Vifungu hivi vinatusithibishia, au vinatuweka wazi kabisa kuwa  farao naye alikufa katika yale maji, japo katika  habari ya farao haijaweka wazi kama farao alikufa naye katika bahari lakini kwa vifungu hivi tu vinatuthibitishia kuwa  naye alikufa katika bahari ya shamu

Mfano ukisoma hapo, kutoka 15:19 mwanzoni hapo anasema'”
Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda  farasi wake waliingia ndani ya bahari” ikituonyesha kuwa farao naye alikuwepo katika msafara huo.

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *