Usiwavunje wengine moyo na usiwasikilize wavunjao moyo na kukatisha tamaa.!

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Kila siku unaposoma maandiko hususani katika maandiko siku zote tembea na neno hili.  “

1 Wakorintho 10:11“Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.”

Unaposoma Habari za wana wa Israeli jifunze kutoka kwao katika yale yaliyowapata kutoka Misri kwenda kaanani. Safari ya Misri kuelekea kaanani ilikuwa ikifunua au ilikuwa ni kivuli kuhusiana na sisi waenda mbinguni. Yale yaliyowapata yote ni maonyo kwetu sisi ili na sisi tusiyarudie.

Sasa katika nyakati hizi za Mwisho yameibuka mafundisho potofu na ya uongo ambayo yanawakatisha watu wengi sana tamaa na kuwapumbaza jambo ambalo ni hatari sana.

Na jambo kama hili pia lilitokea kwa wana wa Israel na ndio likapelekea umati mkubwa jangwani kuangamia wanashindwa kufika kaanani.. kama maandiko yanavyosema…..

Hesabu 32:9“Kwa kuwa walipokwea na kuingia bonde la Eshkoli, na kuiona nchi, wakawavunja mioyo wana wa Israeli, ili wasikwee kuingia nchi Bwana aliyowapa.”

Ukisoma vizuri Hesabu 14:1-11. Utaona baada ya wale watu waliokuwa wametumwa kuipeleleza nchi ya kaanani baada ya kuiona yote walirudisha majibu mbele ya Musa na haruni na mbele ya kusanyiko la wana wa Israeli kuwa nchi ile kweli ni nzuri sana lakini watu waliokuwa wanakaa humo ni hodari na wakasema hata walijiona kama mapanzi na wakasema tena hawataweza kabisa kuingia humo maana yake watakufa wakijaribu kuitwa ile nchi ya Kanaani.

kana kwamba Bwama aliwaahidia uongo lakini Bwana aliwaambia ukweli kabisa walipaswa kumtazama yeye tu na wala si uhodari wa wale watu waliokuwa wanakaa mle..

Taarifa hizi zilileta taharuki kubwa katikati ya kusanyiko lote la wana wa Israeli na ndio hapo watu wakaanza kutamani kurudi Tena Misri na wakafikia hatua kidogo sana Musa na Haruni wauwawe na ule mkutano kwa Mawe. Ndipo Bwana alipotokea na zoezi lile likasitishwa.. lakini tunasoma watu wawili kati ya wale waliotumwa kwenda kuipeleleza nchi ile wao waliona hali halisi kweli lakini walimwamini Mungu kuwa atawapa ile nchi. Nao ni Yoshua na Kaleb..

Tunajifunza nini katika hii Habari?

Leo hii kuna kundi kubwa sana la watumishi wa uongo wana wa Ibilisi wanaowakatisha watu tamaa kwa kuwahubiria injili za uongo.

Leo hii watu wanahubiriwa kuwa “HAIWEZEKANI KUISHI MAISHA MATAKATIFU “ yaani kwa maana nyingine utakatifu ni kitu ambacho hakiwezekani.. kana kwamba Yesu alisema Uongo katika Mathayo 5:48, na 1 Petro 1:16 nk. Watakuhubiria zaidi msamaha wa dhambi tu na mafanikio ya mwilini tu..nk

Wanawaaminisha kuwa matendo mema kwa mtu alieokoka si lazima kuyafanya na kama mtu alieokoka akiwa ni mtu wa bidii sana kutenda matendo mema sawa sawa (Waefeso 2:10) watakwambia….

“Unapambania wokovu” au watakabia wewe ni “Mwokozi mwenza” nk hivyo kumvunja moyo Mkristo anaefanya juhudi katika hayo na aone kumbe haina maana na aone kwamba yeye hajui na amepotea kumbe ni uongo wa ibilisi.

Leo hii utasikia injili kama hizo zinakwambia ukishaamini tu basi inatosha wewe unaenda mbinguni umeshapigwa mhuri wa Mungu hupotei hata ufanye nini.. msalabani kazi iliishaa….

Ni kweli msalabani kazi iliisha lakini haikuisha ili kuhalalisha uovu. Au kukupa uwanja wa kuishi unavyotaka lakini sivyo.. kumbuka unapomwamini Yesu Kristo unafanyika kuwa ni mtoto wake na kama mtoto ni lazima ufate kile baba yako anachokwambia.. na huwezi kujiamlia chochote…

Na pia maandiko yanasema..

Yohana 10:27“Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.”

Siku zote lazima utaisikia sauti ya Mchungaji wako Yesu Kristo inakutaka ufanye nini.. lazima uwe chumvi ya ulimwengu, na kamwe kuvaa kwako,kuongea kwako,mwenendo wako nk lazima uwe tofauti kabisa na ulimwengu huu ikiwa ni mwanamke lazima Sauti itakuongoza na Roho Mtakatifu atakukumbusha acha kupaka hayo ma lipstick,Makups,kuvaa suruali,mawigi,vikuku,kupaka kucha rangi na kwenda kwa ma master kucha kushikwa hiyo miguu na mikono nk.

lazima Roho Mtakatifu atakushudia ikiwa kweli umedhamiria kumfuata Yesu Kristo lakini kama upo kupoteza Muda hutasikia na utaendelea na kusema uko chini ya neema na mwisho wa siku utaangamia pale Bwana atakwambia sikujui utokako..

Maanisha kweli kumfata Yesu Kristo.. jikane mfuate Kristo.. acha kujitumainisha katika uongo.

Kumbuka wana wa Israeli katika safari yao tafakari vizuri walikuwa watu zaidi ya 2 million kutoka Misri na katika wale walifika 2 tu kaanani.

Ni maombi yangu kwa Bwana wangu Yesu Kristo akupe neema kila siku ya kupiga hatua na kuendelea mbele Kataa mtu anaekwambia utakatifu sio lazima,umeokolewa umeokolewa milele… epuke huo ni uongo utakuwa huna tofauti na mke wa Lutu.

Kumbuka wana wa Israeli wote waliokolewa kutoka Misri lakini wengi hawakufika kaanani. 1 Wakorintho 10 yote Soma..

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *