
INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.
(Ujumbe kwa wanawake wote)
Mathayo 7:13 “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.”
Wapo wanawake wengi ambao wanapita kwenye mlango mpana lakini wanajiona kuwa wanapita kwenye mlango mwembamba…na walio kama hao ni wabishi na wanajifanya wajuaji sana wa Neno la Mungu, na hata ukijaribu kuwaelewesha bado watakataa.
Wanawake wanaopita kwenye MLANGO MPANA huku wanajiona wanapita kwenye mlango mwembamba wanatambulika kwa..
-Matendo yao
-Ongea yao
-Vaa yao
-Tabia yao
Mlango mpana ni njia inayokupeleka moja kwa moja KUZIMU.
Na njia hii wanaipenda wengi sana maana haina sheria, amri, majaribu, changamoto n.k, yaani wanaishi jinsi wanavyotaka wao, na si jinsi MUNGU anavyotaka,
Mfano mwanamke anayetumia mapambo yoyote yale na kuvaa vimini, suruali, nguo za kubana, kujichubua, marasta, mawigi, kusuka NYWELE, kupaka rangi NYWELE, kucha rangi, na uchafu WOWOTE wa mwilini, pamoja na uchafu wate wa MOYONI, yaani kiburi, dharau, umbea, chuki, majivuno, uchoyo, ulafi, MASENGENYO, wivu, uongo, wizi, uuaji, uzinzi, uasherati, vinyongo na mengineyo.
KAMA UNAFANYA HAYO, HATA ULITAJE JINA LA YESU MARA ELFU… UJUE UNAPITA KWENYE NJIA PANA IENDAYO UPOTEVUNI. Geuka na uache leo, ubadilike ili YESU KRISTO apate kukuonyesha njia nyembamba na akuwezeshe kupita ili uende kwenye njia ya uzima wa milele MBINGUNI.
Lakini mlango ni mwembamba na njia finyu ielekeayo kwenye uzima na ni wachache tu waionao. (Mathayo 7:14)

Bwana akusaidie ewe Binti/Mwanamke ili uchukue hatua ya kubadilika.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.