Ipi tofauti kati ya kifo na mauti?

Maswali ya Biblia No Comments

 

Kifo ni Hali ya kutoka uhai ndani kwa kiumbe chochote , na kinaweza kumtokea Mwanadamu,mnyama, mmea, kwa kuwa ndani yao umo uhai basi vinapotokwa na huo uhai vinakufa..

Mauti  ni kifo pia ijapokuwa mauti ipo kwa wanadamu, kwasababu hakuna uhalisia wowote kusema mti umekumbwa na mauti, au paka amekumbwa na mauti, bali sentensi kamili ni, paka amekufa,mti umekufa, anayekumbwa na mauti ni mwanadamu tu.

Sasa kwanini kifo kiwe tofauti na mauti?

Hiyo ni kuonyesha uzito wa hiyo hali kwa mwanadamu, mfano wa “kilio”  kinaweza kutokea kwa mkubwa hata mdogo, lakini kwa mtu mkubwa kitachukulika kwa uzito zaidi, ni kama misemo ya kijamii isemavyo,ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo” ikimaanisha ukiona mtu mzima analia fahamu hapo kuna uzito wa hilo jambo..

Pengine anapitia changamoto kubwa asizoweza kuzitatua, labda ni magonjwa makubwa, au msiba,kuumizwa moyo sana, kwasababu sio desturi ya mtu mzima kulia, tofauti na mtoto anaweza akalia lakini hana sababu za msingi..

Hata kwa kifo na mauti, Jambo ni lile lile, kuondoka kwa uhai ila linapotokea kwa mwanadamu linakuwa na uzito mkubwa kwasababu tokea hapo mwanzo hakuumbiwa kifo ndani yake, Heshima ya juu na viwango ambavyo Mungu alivyompa mwanadamu, kwa jambo la mauti kumpata ni anguko kubwa sana kwake, ndo mana mauti ikawa ni pigo kwa mwanadamu yoyote…

Sababu ya mauti kumpata mwanadamu ni DHAMBI

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Wanadamu walipomwasi Mungu pale edeni, adhabu iliyotukumba ni mauti, na limekuwa pigo sana kwa wanadamu tofauti na wanyama ambao hawajui chochote kuhusiana na kufa, lakini sisi tumepewa uelewa wa kufahamu kuna siku uhai utaondoka ndani yetu..

Ingekuwa heri kama ni kifo tu cha Mwilini ikaishia hapo, biblia imeezidi kuelezea baada ya kifo, kuna adhabu ya kifo cha roho, na ndo inajulikana kama mauti ya pili, huko ndiko roho zote zitamaliziwa kabisa Katika hilo ziwa la moto, hapo utafahamu kifo alichonacho Mwanadamu na kifo cha mnyama,

Yaondoe mawazo kwamba ukikumbwa na mauti utakuwa kama mnyama tu usiyejielewa, sivyo kabisa” ukiwa mwenye dhambi na ukafa Katika hali hiyo jua utanyoosha moja kwa moja jehanamu, ukingoja siku ya kufufuliwa ifike ili uhukumiwe ukatupwe kwenye ziwa la moto milele,

Lakini habari njema ni kuwa yupo mwanamume mmoja aliyekuja kuikomesha mauti kwa mwanadamu naye ni YESU KRISTO, yeye amwaminiye yeye anatoka Katika mauti na kuingia kwenye uzima wa milele..

Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”.

Umeshuhudia hapo, ukiwa ndani ya Yesu Kristo mauti inakuwa haina nguvu ndani yako, ni wakati wako huu wa kumpokea kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako,unasubiri nini, unajuaje kama kesho utaamka tena,huna garantii ya kuishi milele, jiulize ukifa katika dhambi ni nani atakuponya roho yako, jitathmini sana..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *