Je kuna tofauti kati ya Roho Mtakatifu na Roho takatifu?

Maswali ya Biblia No Comments

 

JIBU:

Hakuna utofauti wowote kati ya Roho Mtakatifu na Roho Takatifu, hilo ni neno moja tu isipokuwa inategemeana kulingana na mahali neno lilipotumika,

Roho Mtakatifu anapotumika ndani yetu, anapozungumza na sisi, na kutuongoza, na kututia katika kweli yote..anachukua nafasi ya mtu wa pili ndani yetu, anakuwa ni kama vile mwalimu na mwanafunzi wake, au baba na mwanaye akimsaidia, akimfundisha, na kumwongoza katika njia sahihi,

hivyo Roho wa Mungu anakuwa kama ni mtu mwingine mpole ndani yetu anazungumza nasi, anatufundisha, anatushauri, anatufariji, anatutia moyo, anatuongoza n.k..Hivyo hiyo tabia ya kuwa kama mtu wa pili ndani yetu, ndiyo inayofanya biblia sehemu zote iitaje Roho ya Mungu, kwa cheo cha uutu. (yaani Roho M-takatifu).

Vilevile tunapomtambua Roho wa Mungu kwa tabia zake ni sahihi kabisa kusema Roho ya Mungu ni Roho Takatifu, ni Roho Nyenyekevu, ni Roho Tulivu, Ni roho Njema (Danieli 5:12) n.k Hapo tunakuwa tumeondoa ule uutu, tunakuwa tumemtaja kulingana na tabia yake ya utakatifu, unyenyekevu, upole, utulivu, n.k,

Hivyo kwa uwelewa huo.. tusifanye mambo kuwa magumu na kuleta mafarakano ndani ya kanisa, kuna madhehebu yanayoleta mafarakano kutokana na haya maneno mawili, utakuta makanisa mengine yamebadilisha biblia zao, kila mahali palipoandikwa kwenye biblia neno Roho Mtakatifu, yamebadilisha na kuweka Roho Takatifu..

Wao wanaona kutumia neno Roho Mtakatifu si sawa, na mengine vivyo hivyo wamebadisha biblia zao kwa kubadili neno Roho Takatifu kuwa Roho Mtakatifu, huko ni kukosa ufahamu..kwa kuwa maneno yote mawili ni sahihi, inategemea ni wapi yametumika.

Fahamu pia kila mkristo ni lazima awe na Roho Mtakatifu kwani maandiko yanasema wale wasio na Roho wa Mungu hao sio wake..kasome Warumi 8:9, na tunapokea Roho Mtakatifu bure kwa kudhamiria kutubu Kwa kumaanisha kuacha dhambi zote kabisa na kubatizwa kwa jina la Yesu sawa sawa na kitabu cha Matendo 2:38

BWANA YESU ANARUDI

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *