Je ni lazima kulipa mahari?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom Karibu tena katika kujifunza neno la Mungu litupalo nuru katikati yetu

Limekuwa swali kwa watu wakitamani kujua kama kweli, upo umuhimu wowote wa kumlipia binti mahari, pale kijana anapotaka kumuoa, na wengine wanajiuliza je Adam alilipa kwa nani mahari ya hawa?

Kwanza kabisa ndoa ya kwanza iliunganishwa na Mungu mwenyewe, Adam asingeweza kutoa mahari maana hawakuwa na wazazi, wao ndiyo walikuwa wanadamu wa kwanza kuumbwa kama tuvyosoma katika maandiko Hawa alipatikana katika ubavu wa Adam, hii ndiyo sababu ambayo Adam hakuweza kulipa mahali

Lakini baada ya uzao kuendelea, ulipaji wa mahari ulinza

Kutoka 22:17
[17]Ikiwa baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa, atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo.

Hata kwa Yusufu pia tunaona alimposa mariamu

Luka 2:4 “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba

Ulipaji wa mahari ni lazima na ni muhimu, kwa sababu ile pesa inayotolewa si kwamba binti anauzwa kwa huyo kijana, si hivyo ila ni jambo la heshima kwa huyo Binti pamoja na wazazi wake, maana pale kijana anamchukua binti wa watu pasipo utaratibu huwa ni jambo la dharau na kukosa heshima na adabu kwa wazazi wa binti na si wao tu hata kwa jamii pia, kwa sababu yule Binti ana wazazi wake kwanini umechukue kiwizi…

Hivyo kijana au unapotaka kuingia katika ndoa hakikisha unafata taratibu zote, hii itakuongezea heshima mbele za Mungu na kwa wazazi wako pia, si jambo la kawaida wewe kijana kukaa pamonja na binti wa watu kabla hamja fata taratibu zote, ukitaka kuota jipange andaaa mazingira mazuri ya kuanzisha familia kisha fata utaratibu mzuri uende ukaoe

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *