JE! UMETOLEWA MISRI?

Biblia kwa kina No Comments

JE! UMETOLEWA MISRI?

Jina la Mwokozi Yesu, libarikiwe.

Karibu tujifunze maandiko, Neno la Mungu wetu ambalo ndio taa iongozayo miguu yetu, na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).

Safari ya wana wa Israeli kutoka Misri, kuelekea Kaanani, ni ufunuo kamili wa safari yetu ya Kristo kutuokoa katika dhambi na kutuingiza katika Neema ya wokovu. Musa anafananishwa na Kristo.. Kama vile Musa alivyowaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, kwa ishara na miujiza Mingi aliyokirimiwa na Mungu, ndivyo Kristo alivyodhihirishwa kwetu kutuokoa kutoka dhambini, kwa ishara na miujiza mikubwa kuliko ile ya Musa. Sasa ni kwa namna gani safari ile ya wana wa Israeli imefananishwa na safari yetu ya wokovu, unaweza kusoma binafsi kitabu cha 1Wakorintho 10:1-12.

Lakini swali la msingi ni je! umetolewa Misri au bado unatumikishwa na Farao?

Huwezi ukasema umetolewa katika utumwa wa dhambi na bado unasujudia sanamu, huwezi ukasema umetolewa katika utumwa wa dhambi na bado ukawa mwasherati, au mlevi, au mtukanaji…Huwezi ukasema umeokolewa kutoka katika utumwa wa dhambi na bado unavaa nguo zinazoonyesha maungo yako, unavaa nguzo zinazo kubana, unavalia vimini, suruali na kupaka wanja..Hizo zote ni tamaduni za miungu ya ki-Misri na huwezi kumtumikia Mungu wa kweli kwa tamaduni za ki-Misri.

Ndugu yangu kama unataka kwenda na Bwana, mtii anayokuambia leo, Geuka upate ufahamu, usidanganyike kwamba Mungu anaangalia roho haangalii mwili, usidanganyike kwamba wanaopaka lipstick,na wanja na wanaovaa hereni, na wigi wataingia mbinguni..Usidanganyike kuwa wanaofanya masturbation, na wanaotazama pornography, na wanaoishi na wanawake/wanaume ambao hawajaoana kuwa wataingia mbinguni, usidanganyike kuwa ukiwa vuguvugu, nusu Mungu nusu ulimwengu, utaingia mbinguni.. Bwana anasema mwenyewe kuwa ATAKUTAPIKA!! Kwasababu yeye ni mtakatifu na hivyo tutakuwa watakatifu kama yeye alivyo.

Na jambo lingine la kufahamu ni kuwa tunapotoka Misri tunatoa pia mioyo yetu huko.

Watu wengi wanadai wameokoka lakini mioyo yao bado ipo katika dunia (Misri).

Ndugu Dada/kaka.. kumbuka unapookoka, ni sawa na umeanza safari yako ya kutoka Misri, au Sodoma… Ulimwengu huu umefananishwa na Sodoma na Misri (Ufunuo 11:8). Hivyo hatuna budi kutoka Misri kweli kweli kwa miili yetu na mioyo yetu!.. sio tu kwa miili bali pia kwa mioyo yetu!.

Maana yake ni kwamba tunapomkiri Yesu, hatuna budi tuukatae ulimwengu kimwili na kiroho, tunapaswa tuache ulevi, mwilini na rohoni, tunapaswa tuache uasherati wa mwilini na wa rohoni, kama Bwana alivyosema katika…

Mathayo 5:27 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;

28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”.

Hivyo tukisema hatuzini tu, na huku mioyoni tunaziwasha tamaa, hapo bado mioyo yetu ipo Misri, ijapokuwa kimwili tumetoka Misri, Tunapookoka na kusema si wauaji, si watoaji mimba, lakini mioyoni mwetu tunavinyongo na chuki kwa ndugu zetu na adui zetu, sisi bado ni wauaji tu (Mathayo 5:21-22) na bado tupo Misri kiroho, ingawa kimwili tunaelekea kaanani ambayo hatutaifikia..

Kadhalika ukiwa Misri na moyo wako upo kaanani, hapo bado upo Misri, haikusaidii chochote! Unapaswa utoke Misri, maana yake ni kwamba upo katika ulimwengu lakini una hamu ya kufika mbinguni, kila siku unasema siku moja nitaokoka, siku moja nitabadilika, siku moja nitaacha kuvaa vimini, siku moja nitaacha kujiuza, siku moja nitaacha ulevi.. Fahamu kuwa hiyo siku haitafika, na utakufa ukiwa bado Sodoma. Huu ni wakati wa kujiokoa roho zetu. Kwa kuamua kuokoka kweli kweli na si kuwa vuguvugu. Kwasababu Bwana alisema watu wote walio vuguvugu atawatapika watoke katika kinywa chake.. (Ufunuo 3:15)

Bwana atusaidie tuokoke kweli kweli, tutoke Misri na Sodoma kiroho na kimwili..

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *