Jitambue uko katika kundi lipi?

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya mwokozi wetu.

Kama Mkristo uliyeokoka ni muhimu sana kujitambua uko katika kundi lipi.? Yapo makundi ya aina Tatu ya Wakristo na katika makundi makuu haya matatu kila moja lina tabia zake na sifa zake.. kupitia sifa hizi naimani utaweza kufahamu upo katika kundi lipi na nini unatakiwa kufanya. Hivyo sifa za Wakristo hawa ndio zinaowatambulisha..

Fahamu unapoitwa Mkristo maana yake wewe umekubali kumfata Yesu Kristo yaani mwanafunzi wa Yesu Kristo na Kristo ndio Mwalimu wako na huna budi kubadilika na kumfata mwalimu wako anataka nini.. hivyo unaposhindwa kumfata unakosa sifa ya kuwa mwanafunzi wake.

Basi tutakwenda kuyatazama makundi haya matatu ni yapi na watu waliopo katika makundi hayo wanasifa zipi?.

1.Wakristo wa mwilini.

2.Wakristo wachanga.

3.Wakristo wa Rohoni. 

Tutaangalia kundi moja baada ya lingine na tabia/sifa za kundi moja moja.

1.Wakristo wa Mwilini.

Hawa ni Wakristo ambao wamedumu kwenye wokovu kwa muda mrefu lakini hakuna mabadiliko/badiliko lolote ndani yao(hakuna badiliko la kweli ndani yao) ni wale wale tu.. tabia za mwilini ndio zimetawala ndani yao. Hii yote ni kutokana na uvivu wa kutokutaka kupiga hatua yaani kujifunza. Unapita muda mtu yuko kwenye wokovu miaka 3 mpaka 5 yupo vile vile tu.

Waebrania 5 11 Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.

12 Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.

Hawa ni Wakristo ambao ni wavivu wa kujifunza. Hawataki kupiga hatua japo kila siku wanakwenda kanisani. Wanataka siku zote wawe ni watu wa kufundishwa tu tena yale mafundisho mepesi ya mwanzo kabisa kama waongofu wapya.

Ukiona umekaa kwenye wokovu kwa muda wa miaka 3 nk na huwezi kuwafundisha wengine/kuwahubiria wengine ni ishara ya kuwa mvivu rohoni na ni mchanga na mbinafsi pia.”

Sifa/Tabia za Wakristo wa Mwilini.

Ziko tabia nyingi sana lakini tutaangazia chache tu kwa leo.

1.kulipiza kisasi.

Wakristo wa namna hii wanakuwa wepesi kulipiza kisasi.. wakitukanwa nao hurudisha matusi, “utasikia naweka wokovu pembeni kwanza…”

ndugu wokovu hauwekwi pembeni harafu baadae unachukuliwa. Wakipigwa nao wanarudisha utasikia “ngoja nimkomeshe.”

Mtu ambae ni adui yake(kwa mtazamo wake yeye anaona ni adui lakini kiuharisia Mwanadamu hana adui ambae ni mwanadamu.. adui wa mwanadamu ni dhambi inayomdai mauti aende kuzimu na Shetani) hivyo akisikia kapatwa na shida anashangilia na kufurahi na anafanya sherehe..

Wakati neno linasema..

Mathayo 5.43  Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

2. Wanakuwa na sura mbili ya kanisani(utakatifu) na mitaani(kawaida).

Wakristo wa namna hii wana sura mbili wakiwa kanisani wanavaa nguo za heshima wakiwa mitaani wanavaa vimini,milegezo. Wakiwa kanisani salamu ni “Bwana Yesu asifiwe “ wakiwa mitaani midomo yao imejaa matusi tu na lugha za kihuni.

Wakiwa mitaani ni vigumu kuwatambua kam ni Wakristo maana wanafanana na aatu wasiomjua Mungu Katika semi nk.

3. Hawapendi kuonywa/kukemewa pale wanapokosea.

Wao wanapokosea hawataki mtu awaambie umekosea wao wanaona wako sawa tena wakati mwingine wanasema “nimekaa kwenye wokovu muda wote huo utaniambia nini wewe ambe umeokoka juzi juzi hapa.” Au hata mchungaji anaposema jambo utasikia “huyu nae anajiona kama kanisa ndio lake nk” hata kama ni kitu cha msingi. Na neno limetutaka tuonyane.. Warumi 15:14.

2.Wakristo wachanga.

Hawa ni wale ambao wanakipindi kifupi sana katika wokovu kama kuanzia siku 1 hadi mwezi 1 mpaka hata miezi 5.

Hawa wanapaswa kukaa katika fundisho la awali kabisa la wokovu. Ili waweze kuukulia wokovu kama maandiko yanavyosema..

1 Petro 2:2“Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;”

Sifa/tabia za Wakristo Wachanga.

1.Wokovu ni faida yao ila hupenda kubembelezwa.

Ni watu ambao wanahitaji kufatiliwa sana na inahitajika hekima katika kuendana nao. Hawahitaji kukalipiwa sana na wanabembelezwa maana wanakuwa bado ni kama watoto ni wepesi kuzila nk.

2.kuomba na kusoma neno mpaka wakumbushwe.

Wao kama wao hawana muda wa kusoma neno wala kuomba si kwamba wako busy muda wote la! Lakini wanahitaji kukumbushwa kumbushwa wanakuwa hawajui vyema umuhimu wa maombi na neno. “Ukiwa umekaa kwenye wokovu kwa muda mrefu na unakumbushwa kusoma neno na kuomba uko katika kundi hili”.

3. Wanakuwa na utu wa kale.

Ukiwatazama kuna Vimelea bado vimo vya utu wa kale utakuta hata wanasikiliza mizi ya kidunia. Wanakaa kubishana na kuchangia mambo ya mipira ambayo haina faida kabisa kwa Mkristo. Nk

4. Ufahamu wao wa Kiroho unakuwa bado ni mchanga.

Watu hawa wanakuwa hawana uwezo wa kupambanua vizuri jambo baya na zuri katika mambo ya rohoni.  Kama vile mtoto asivyoweza kupambanua vyema mambo ya mwilini kama mtu mzima nao wanakuwa hivyo hivyo. Watakwambia hata..

kwani kuangalia mpira ni dhambi? Au kuweka mawigi, makucha ya bandia ni dhambi? Au kuvaa suruali kwa mwanamke ni dhambi?, nk ” ni kwa sababu upambanuzi bado haujaingia ndani yao vyema wanahitaji kufundishwa taratibu mwisho watapevuka hawatauliza tena wataacha wenyewe tu.

3. Wakristo wa rohoni.

Hawa ni Wakristo walioamua kweli kweli kujikana nafsi na kumfata Yesu Kristo na neno la Mungu limebadilisha maisha yao kabisa na wamefanana kweli na mwokozi. Kila siku wanazidi kupiga hatua na wanazidi kuwa na maarifa mengi zaidi kuhusu Yesu Kristo.

Ni watu ambao imani walioipokea ndani yao inazaa matunda. Katika mwenendo wa upendo,kuhubiri injili nk.

Sifa/Tabia za Wakristo wa Rohoni.

1.Mungu ni wakwanza katika maisha yao.

Ni Wakristo ambao wanajishughulisha sana na mambo ya Mungu na wanampa Mungu nafasi ya kwanza sio watu wa udhuru udhuru, ni watu wanaojitoa kweli kweli. Wapo radhi kupoteza hata kazi zao kuliko kupoteza ushirika wao na Mungu.

Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.“

Ni watu ambao wanawekeza sana katika kutafuta mambo ya rohoni. Kuliko mambo ya mwilini “si kwamba hawatafuti mambo ya mwilini kama Fedha nk ila mioyo yao na Muda wao mwingi hauko huko.”

2.Ni watu wa matunda.

Wakristo wa namna hii huzaa matunda maana ndio kusudi la kuitwa kwao. Wanamzalia Mungu matunda ya kazi(kuhubiri injili) lakini pia matunda ya haki(Wagalatia 5:21-22) ambayo ni upendo,uvumilivu,Fadhili, uaminifu nk.

3.Wamekubali kuongozwa na Roho Mtakatifu wala hawayafati mambo ya mwili(tamaa za mwili).

Ni watu ambao wamekubali kuongozwa na Roho.

4.Wanailinda sana imani yao kuliko kitu kingine kile.

Ufunuo 2:25.

5.Mahali popote hujulikana kuwa wao wameokoka hata kabla hawajajitambulisha.

Ni Wakristo ambao wakiingia mahali popote wanajulikana kabisa kuwa wameokoka. Hawahitaji kujitambulisha.

Wakifika sehemu hata kama watu hao wanaongea lugha chafu na mizaha watu hao hukaa kimya maana wao ni nuru na siku zote giza haliwezi kukaa pamoja na Nuru ni lazima Nuru itawale tu.

Naimani kupitia makala hii umejifahamu upo katika kundi lipi? Ikiwa uko la kwanza piga hatua ufike kundi la tatu ikiaa uko la pili piga hatua utike kundi la tatu na ukiwa uko katika kundi la tatu endelea sana zaidi ya hapo ulipo. Fahamu tuna muda mchache.

Chukua hatua leo hii ya kupiga hatua ufike kundi la tatu. Usilidhike na mahali ulipo.Jitafakari vyema kisha chukua hatua ubarikiwe sana..

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *