Kaa mahali ambapo Mungu amekusudia uwepo!.

Biblia kwa kina No Comments

Kaa mahali ambapo Mungu amekusudia uwepo!.

Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Mahali ambapo Mungu amepakusudia kwa kila mtoto wake kukaa na kukuzwa ni sehemu moja tu nayo inaitwa kanisa.

Agenda au mkakati wa Mungu kukutengeneza na kukuimarisha kiroho lakini pamoja na kuwakomboa watu kutoka gizani na kuja Nuruni vyote kwa pamoja vinafanyika katika kanisa.

Kanisa ni mkakati/agenda ya Mungu duniani. Kanisa linamuwakilisha au kumdhirisha Mungu duniani, Mungu hadhihirishwi mahali popote pale ila ndani ya kanisa maana ndio utendaji kazi wa Mungu ni ndani ya kanisa.

Na kanisa ninalozungumzia si jengo bali ni watu waliomuamini Yesu Kristo walio na Roho Mmoja,Baba mmoja na ni mwili mmoja na ubatizo mmoja pia.

Kanisa ni familia ya Mungu duniani/ufalme wa Mungu duniani. Kama Mkristo usipofahamu kanisa ni nini na kwa nini unatakiwa kushikamana sana na kanisa basi upo katika hatari yaani hauko salama.

Wakristo wengi duniani wanachukulia kanisa ni sehemu ya kwenda tu kukutanika kumsifu Mungu, kusikiliza neno na matangazo baada ya hapo kila mtu anaendelea na mambo yake.

Ndugu yangu kanisa ni zaidi ya hapo. Ikiwa unaliona kanisa katika picha ya namna hiyo basi upo hatarini na haujui hasa kanisa ni nini!?.

Baada ya kuzaliwa mara ya pili kama mtoto Mungu lazima akuweke katika familia yake(hilo kanisa ulilopo kwa sasa) na kitu Mungu anachokusudia kukiona kwako ni kuona unawajibika kama mtoto katika familia kwa kuhudumia wenzako katika kile ambacho Mungu amekiweka ndani yako. Na kuhusika katika shughuli mbalimbali za kifamilia.

Leo hii kuna Wakristo wengi hawajui au kufahamu wajibu wao katika kanisa, wanasubiri mpaka waambiwe fanya hiki na hiki na wanafanya kwa kujisikia.

Leo hii Mkristo anakwenda kanisani jumapili kwa jumapili hawezi kufika katikati ya wiki kwenye mafundisho ya biblia au katika mikesha. Na hakuna sababu ya msingi inayomzuia kutokufika ni basi tu. Ndugu haijalishi umeabudu kanisani hapo ulipo kwa miaka 10 kama wewe ni wa jumapili kwa jumapili wewe sio mwanafamilia wa hilo kanisa.

Wewe ni mtembeleaji wa hilo kanisa na wala si Mshirika na ndio maana huna mzigo wowote ndani yako kuhusu kanisa, huna mzigo wa kuwaombea wenzako,wala kuwafundisha wala kuwa na ushirika nao wa karibu na kila kitu kwako kuhusu kanisa ni mzigo huoni hata kiu ya kuliombea kanisa ukiwa mwanafamilia lazima kuna mzigo ndani yako utaumbika tu juu ya kanisa Mungu atauweka ndani yako.

Kanisa ni mwili wa Kristo na mwili wa Kristo unavyo viungo mbali mbali na vyote vinawajibika kwa sehemu yake je wewe unawajibika mahali popote katika mwili wa Kristo?.

Waefeso 4

15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.

16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja,huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.

Unaona hapo? Anasema “ kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja,….” hasemi kwa kadiri ya kila sehemu nyingi nyingi la!, ikiwa na maana mwili wa Kristo unajengwa na sehemu moja baada ya nyingine.

Ni sawa na nyumba haijengwi na tofari moja bali ni muunganiko wa tofari nyingi na kila tofari inakaa sehemu yake, na kama ikitolewa moja au ikiharibika moja mahali ilipowekwa kutakuwa na uwazi ambao unaweza kuingiza vitu visivyofaa kama nyoka nk.

Vivyo hivyo wewe usipokaa katika nafasi yako katika kanisa unaliadhiri kanisa kwa sehemu,  ilikubidi uwe muinjilisti,muimbaji,nk lakini haupo katika sehemu yako,

Unaenda kanisani kwa kujisikia leo uende au la!, ni mtu wa kuhama hama makanisa leo uko hili kesho lile keshokutwa lingine ndugu hutakua kiroho na matokeo yake utadumaa kabisa na kufa kiroho.

Acha tabia ya kuhama hama makanisa tulia hapo Muombe Mungu akusaidie ujue kusudi lako hapo na ikiwa bado hujafahamu shiriki kikamilifu ikiwa ni katika usafi,nk Mungu atakuonyesha huko huko karama yako ukiwa katika kutumika sio katika kutulia.

Na makanisa mengi yamepoa katika eneo la mambo ya Ki-Mungu utakuta kanisa lina ratiba mbili tu, jumapili ibada na Mkesha basi kwa wiki yote.

Na wakati mwingine Mkesha mara moja kwa mwezi(tena mwisho wa mwezi,  nani kukwambia  mkesha unatakiwa ufanyike mwisho wa mwezi tu)hapo kama kanisa ikiwa wewe ni kiongozi wa kanisa yaani mchungaji, askofu nk hutengezi watu ambao wanaweza kusimama na kuitetea injili yaani watu wanaoweza kuangusha ngome.

Kama mchungaji weka ratiba angalau mara tatu kwa wiki au mara 5 mnakusanyika ikiwa ni maombi nk hapo utaweza kuwatengeneza wakina Paulo wengi, mchungaji usiwe mzembe na mzito kunbuka ni wajibu wako na utatoa hesabu siku ile.

Na wewe mwanafamilia wa kanisa hilo ulilopo jitahidi kufanya ushirika wa kudumu katika roho, leo hii ushirika kwa Wakristo wengi ni katika vipindi vya sherehe tu yaani harusi nk.

Mnapokosa ushirika(lengo ushirika kukutana mara kwa mara kuombeana,kufundishana,kuonyana,kupendana zaidi ya ndugu wa damu nk ni kuimarishana kiroho na kuchungana.)

Mambo kama haya yanapokosekana kwa wingi ndio hapo kunakuwa na ubaguzi,kuoneana wivu,maseng’enyo,majivuno nk. Lazima mambo kama haya yawepo katika kanisa kama kanisa litakosa mambo hayo hapo juu. Inapelekea kuharibu taswira ya kanisa.

Rudi katika kitabu cha matendo ya mitume kisome chote wewe mchungaji na wewe mwanafamilia wa kanisa hilo(si mtembeleaji ambae ni wa jumapili kwa jumapili). Angalia kwa nini kanisa hilo lilukuwa na mafanikio sana nje na ndani pia.

Matendo ya Mitume 2

42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

43Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume.

44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika,

45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.

46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,

47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

Angalia hawa watu! Walikuwa wakidumu katika fundisho kwa muda mrefu maana yake hakuna fundisho liliokuwa linawapita,walikuwa wakifanya ushirika mara kwa mara na mambo hayo yalizaa upendo kiasi kwamba mtu alikua radhi kuuza mali zake kwa ajili ya kuwasaidia wenzake katika kanisa.  Leo hii kanisa limejaa ubinafsi tu. Mungu atusaidie sana.

Leo hii Mkristo hawezi kukaa katika ibada kwa masaa 6 mpaka saba ni lisaa limoja basi tena la kusikiliza neno, unafikili hapo tutapata watu kama wakina Timotheo, Paulo,Sintike nk?

Ni uongo watu walikaa zaidi ya siku tatu wakimsikiliza Bwana Yesu bila kula,watu walikaa usiku kucha wakimsikiliza Paulo mpaka wakina Eutiko wanaanguka madirishani,watu walikaa wakashuhudia wakina anania na Safira wanakufa wote anaanza Anania alikuja ibada ikiwa inaendelea akadanya akafa, akaja mke wake baada ya saa tatu watu walikuwa wanaendelea na ibada nae akafa na bado wakaendelea na ibada.

Leo ikifika saa7 mchana tu mtu anaona mahubiri yamechelewa kuisha anaondoka na anaenda tu kufanya mambo yake amabayo hata asingefanya yansingekuwa na hasara. Na tunakaa tunamsubiria Yesu kweli???

Badilika kaa katika familia yako,penda ibada,penda kanisa lako(ndugu zako katika Kristo) nk.

Maranatha.
@Nuru ya upendo.
Mawasiliano:0613079530.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *