Kama shomoro katika kutangatanga kwake( mithali 26:2)

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana wetu Yesu Kristo na Asifiwe sana.

Ukisoma kitabu cha  Mithali 26:2 ili maanisha nini?

“Kama SHOMORO katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.”

Jibu: Laana zisizo na sababu Mungu anazifananisha na Shomoro au ndege wanao Tanga-tanga angani.

Jamii mbalimbali za ndege huonekana angani kila siku wakiwa bize na shughuli zao mbalimbali lakini kamwe hawana habari au madhara yoyote kwa binadamu, hata kama angewaudhi kwa kuharibu viota vyao, kuwapiga mawe, hawatoshambulia maana hawana Uwezo! Hata mwanadamu akiwaona hawezi kuwaogopa pia, ni tofauti na nyoka ambae akimwona, atajihadhari Asimwume.

Sasa Je! Mungu anasema Habari za ndege?

La! Hapo tunafunuliwa kuhusu LAANA ZISIZOKUWA NA SABABU kuwa haziwezi kukupata Wewe ulie Mtakatifu wa Mungu; Bali zitakuwa ziki tanga-tanga kama ndege wa angani katika shughuli zao kutwa. Hivyo kumbe kama mwamini huna sababu ya kuogopa-ogopa laana au Maneno yasiyo na sababu.

Ukiona laana fulani imekupata basi kunayo sababu nyuma yake, lakini si kwa maneno matupu! Mfano wa laana isiyo TUPU ni pale Elia alipowalaani wale vijana 42 Walioliwa na Dubu SABABU Walimdhihaki (2 Wafalme 2:22-25)

Mfano wa laana TUPU ni Ile ya Mchawi Balaam dhidi ya Waisrael, maana hawezi laani Wabarikiwa (Hesabu 23), Nyingine ni ya Goliati dhidi ya Daudi kwa miungu yake ya kifilisti, hakika ilikuwa ni laana ya Bure! Soma..

1 Samweli 17:42″ Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. 43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake”

Hata sisi leo Hatupaswi kuogopa laana za waganga au wanadamu kwa maana tu Wabarikiwa! Ni kitu cha ajabu Mkristro kutetemekea laana za wazazi au nduguze eti kwa sababu kaokoka au kakataa Matambiko?!, au Mchawi kamwambia tu “wewe kesho hutaiona!”
Sikiliza Mpendwa, hizo ni laana tupu, wewe Ishi katika imani ukiamini hizo ni Shomoro tu angani katika taabu zake za kutwa, hazitokudhuru kamwe!

Ukiokolewa na Bwana Yesu Kristo, Basi u Mbarikiwa; wewe ni uzao wa kifalme, Ngome imara Isiyoangushwa, Jeshi la Yesu Kristo Tena Anaishi ndani yako, Uogope Nini? JE ni laana tupu za Binadamu? Tambua mamlaka na Nguvu ulizopewa katika Kristo. Na laana zitashindwa hakika!

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *