
Kama shujaa wa Bwana ni lazima uwe na uso kama wa Simba.
Jina kuu la Bwana YESU KRISTO Mkuu wa Wafalme wa dunia na Simba wa kabila la Yuda libarikiwe milele yote. Karibu tujifunze injili ya kweli.
Kama tunavyojua simba ni mnyama jasiri asiye na woga, biblia inasema katika..
Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.
30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;”
Kama shujaa wa Bwana ni lazima uwe na ujasiri kama simba, hupaswi kuwa na hofu wala mashaka yoyote, au kutishiwa na kitu chochote. Simba hatishiwi!!
Wale mashujaa wa Daudi kutoka katika kabila la Wagadi walikuwa na nyuso kama nyuso za simba walimwendea Daudi kwa ujasiri wote, na sisi ni vivyo hivyo.
1Mambo ya Nyakati 12:8 “Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;
Mkristo, ni lazima uvae sura ya ujasiri kwa ajili ya imani yako na injili, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyokuwa, na ndio maana anaitwa Simba wa Yuda (Ufunuo 5:6). Yeye hakuogopa mwanadamu yoyote, ilipofika suala la wokovu hata Herode alipotaka kumkamata, aliwaambiwa wale watu akisema “mwambieni Yule MBWEHA”!.. kuonyesha kuwa yeye hababaishwi na mwanadamu yoyote kuhubiri injili.
Vilevile na sisi ni lazima tuwe kama simba tukiwa hapa duniani kwasababu shetani naye hatufuati kama kondoo, bali kama Simba, biblia inasema hivyo katika 1Petro 5:8, Unategemea vipi na sisi tumwendee kwa upole katika kuuharibu ufalme wake?
Hivyo kama mkristo uliyeokoka kweli kweli, fahamu kuwa we ni shujaa wa Bwana Yesu, pasipo kujalisha jinsia, umri au elimu uliyonayo kumhusu Mungu.
Kuanzia leo jivike ujasiri wa kumtumikia Bwana pasipo kuogopa kitu chochote, usiangalie vitisho vya adui, wala usisikilize mawazo ya shetani yanayokuhubiria kuwa hujui kuomba, huwezi kuhubiri injili, achana na hayo mawazo kabisa yanayokuambia sauti yako ni mbaya ukimwimbia Bwana, simama kwa ujasiri na uendelee mbele maana Roho Mtakatifu yupo kukusaidia.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.