Maana halisi ya konzi
Ni kipimo chenye ujazo wa kukaa mkono mmoja wa mwanadamu.
Tujifunze zaidi katika maandiko haya yaliyo ainishwa hapa sawa sawa na maandiko ya Bwana yanavyosema.
Mithali 30:4 “Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua”?
Mhubiri 4:6 “Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo”.
Isaya 40:12 “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani”?
Kutoka 9:8 “Bwana akawaambia Musa na Haruni, Jitwalieni konzi za majivu ya tanuuni, kisha Musa na ayarushe juu kuelekea mbinguni mbele ya Farao
Tunaona maana halisi iliyomaanishwa hapa ni mkono mmoja wa mwanadamu ukiwa umewekwa kitu ndani yake au ukiwa mtupu.
Pia tunaweza kuyatafakari maneno haya ya Bwana ili tujifunze zaidi kuhusiana na konzi na tuelewe vile ambavyo Bwana anatufundisha ili tumjue zaidi Bwana wetu Yesu Kristo.
Mhubiri 4:6 “Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo”.
Bwana wetu Yesu Kristo anatufundisha zaidi kuwa heri kuwa na kidogo kutoka kutoka kwa Bwana kilichoambatana na utulivu pasipo mahangaiko kuliko kuwa na konzi mbili na zaidi huku ukiwa hauna utulivu na amani ambapo hupelekea moyo kuwa njia panda yenye mateso na taabu.
Hivyo inatupasa turidhike na kile kidogo tulichonacho kuliko kujitakia vingi ambavyo vitatupa mateso kwakuwa katika vingi watu huwa tayari kufanya uovu ili wapate vingi na mwisho huishia kupata mateso na taabu likini pia inatupasa kuwa makini tunapoongezwa ili tusiishie kuteseka badala yake tuzidi kukabidhi kwa tulivyonavyo ili avilinde na visiwe chanzo cha kuteseka na kutaabika.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.