Shalom karibu tujifunze
Tusome
Mathayo 23:11 “Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.
12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa”
Maana ya kudhili ni kunyenyekea au kuchuka chini, au kushushwa chini
Mathayo 23:11 “Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.
12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa”
Ukisoma andiko tena
Zaburi 75:7 “Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu”.
Hili lilikuwa agizo la Mungu kwa watu wote, ili kumtaka Kila mtu aishi maisha ya unyenyekevu, hata kama una kitu kikubwa kumzidi mwingine jambo ambalo Mungu alilitaka ni kujishusha tu, ndiyo maana mara nyingi tunashuhudia mtu alikuwa na kitu fulani mara kinatoweshwa, Mungu huruhusu ili kumfundisha mtu huyo namna anapaswa aishi ndiyo maana hapo anasema atayejikweza atadhiliwa, lakini atakaye jidhili atakweza
Tusome habari hii tujifunze
Luka 18:9 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”
Mfarisayo alijiona Bora kuliko mtoza ushuru, maandiko yanatueleza wazi, kuwa kati ya mfarisayo na mtoza ushuru walipokuwa katika kuomba, mfarisayo kwa kuwa alijiona bora kuliko mwenzake hapo alijidhili, kama jinsi ilivyo kanuni ya Mungu, mfarisayo alishushwa chini maombi yake hayakuoata kibari, kisha mtoza ushuru kutoka na unyenyekevu wake Mungu alimdhili
Nawe hakikisha unyenyekevu ni sehemu ya maisha yako, uwe Bora au una kitu, au huna jambo analololitaka Mungu ni KUJISHUSHA TU . Usijiinue kabla Mungu ajataka jambo hilo liwe kwako dumu katika unyenyekevu, hata kama ni mwema kiasi gani nyenyekea kwa watu wote
UBARIKIWE
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.