Kuishi kwa neno, ni kuishi maisha ya namna gani?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu katika kujifunza

Kuishi kwa neno, ni sawa tu na kuishi kwa kufuata sheria na mtu anapoishi kwa kufuata sheria ni lazima azijue ili ajue namna ya kuziishi bila kuvunja hata moja mfano wa sheria ya nchi ya Tanzania inasema usile rushwa, au usifanye biashara haramu, sasa kwa mtu anayejua sheria ya nchi yake hawezi kuvunja hata moja kwa sababu anajua akienda tofauti nini kitafata..

Wakati mwingine sheria hiyo hiyo hutumika kupata haki mfano mtu atakiwi kukudhuru, au kukutesa au kunyang’anywa haki yako kwa hiyo kupitia sheria hiyo iinafanya mtu Aishi kwa amani kwa sababu sheria ya nchi yake anaijua

Hivyo hivyo katika Neno la Mungu lazima ulijue kwanza neno la Mungu limeagiza nini, ili ujue namna ya kuishia kulingana na kile kilichoandikwa, neno la Mungu linaposema mwanamke avae mvazi yampasayo, kutozini, kumpenda Mungu kwa Roho, kwa nguvu, kuwaombea wanaokuudhi haya unapasawa uyatiii bila kulazishwa kwa kufanya hivyo unakuwa umeliishi neno la Mungu….

Na katika kupata haki, unatumia neno kujilinda ili upate haki yako, mfano unapokuwa unaumwa unalitumia neno imeandikwa

Isaya 53:5
[5]Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu;
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,
Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Ukilijua kukutumia neno na kuliishi neno hakuna jambo lolote ambalo litaweza kukusumbua katika maisha yako kwa sababu unalijua neno na unaliishi neno

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *