Maandiko yalimaanisha nini kusema kaini alitoka mbele ya uso wa Mungu, JE yaalimaanisha kuwa alikufa au la ?
Tusome
Mwanzo 4:9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. 16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni”
Jambo hili lilitokea baada tu ya kaini kumuua ndugu yake Habili, tukisoma maandiko yanatueleza kati ya laana ambazo Mungu alimpa kaini moja wapo ilikuwa nihii kukaaa mbali na uso wa Mungu
Tunaenda kujifunza ni Kwa namna gani kaini alitoka mbele ya uso wa Mungu
Hapo alipotoka mbele ya uso wa Mungu haimaniishi kwamba ni likufa , au kughahiri mazungumzo kati yake yeye na Mungu, hapana kutoka mbele ya uso wa Mungu kunakomaanishwa ni kwamba (kaini aliachana na habari za Mungu kabisa) yaani habari yake na Mungu iliiishia hapo hapo, akaanza kufata mambo yake mwenyewe, ibada, kutoa dhabihu hizo habari ziliishia pale pale akaanza kufata mambo yake mwenyewe kuvumbua vitu vya dunia tu na kuvifuata, kiufupi uzao wa kaini ulikuwa unawaza anasa na uovu wa duniani hakukuwa na hofu ya Mungu ndani yake soma (mwanzo 4:20-22)
Lakini ilikuwa tofauti kwa uzao wa adamu kwanzia kwa sethi
Mwanzo 4:25 “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. 26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana”.
Tunaona uzao hui ulijishughukisha na kutenda mapenzi ya Mungu, maandiko yanasema wakaanza kuliita jina la Bwana …
Jambo hili linatufundisha nini kwetu pia
Hii roho ya kaini na roho ya kuliita jina la Bwana ipo, na zote mbili zinafanya kazi ikiwa kama utaruhusu mambo ya dunia hii yakutawale, na kuona furaha kabisa kufanya mambo maovu mbele za Mungu, tambua kabisa tayari wewe umetoka mbele za uso wa Mungu … Lakini lipo kundi ambalo linamtumaini Bwana, linamwabudu Mungu, linanyenyekea linafuata sheria ya Mungu hili ndilo kundi ambalo linapaswa kufuatwa na kila mwanadamu
Uchaguzi upo mikoni mwetu mwisho wa mambo yote umeshakwisha kulijulikana, hivyo tujizidi kujitakqsa na kuliita jina la Bwana …
Ubarikiwe
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.