Kwanini Mungu aliruhusu kuua na, sehemu nyingine amekataza kuua

Maswali ya Biblia No Comments

Tusome

Kumbukumbu 13:6 “Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;

7 katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia;

8 usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;

9 MWUE KWELI; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote.

10 NAWE MTUPIE MAWE HATA AFE; kwa kuwa alitaka kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.

11 Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako”

Hapo tunasoma, tunaona Mungu anaruhusu watu kuua , lakini hapa anakataza

Kutoka 20:13

[13]Usiue.

Kwanza kabisa neno la Mungu halijichanganyi ila ni sisi wenyewe katika kuelewa

Agano la kale lilikuwa kivuli cha agano jipya, ndiyo maana mambo mengi katika agano la kale yalikuwa yanafanyika kimwili sana, mfano kutokula wanyama ambao hawacheui, au samaki ambao hawana mapezi, yote haya yalifanyika kimwili, na sheria mbalimbali zilitolewa, na zilitolewa ili waweza kuishi katika mapenzi ya Mungu, japo haikusaidia kwa sababu sheria yao ilikuwa ya mwili, ilikuwa ngumu kuitimiza, lakini katika agano jipya Bwana alilliweka katika uwazi tusome

Mathayo 5:21-23

[21]Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.

[22]Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

[23]Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

Katika agano lililo bora ambalo Kristo mwenyewe aliliweka katika uwazi kuwa yeyote tu atayemuonea mwenzake hasira huyo tayari ni muuaji, kwahiyo hapo agizo kuu Mungu alitakaza tukae katika upendo..

Na jambo lingine Mungu alieleza jambo lolote utakalo mtendea mwezako jua kabisa litakurudia pia

Mathayo 26:51 “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.

52 Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga”.

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *