Maana ya mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake kwa ajili ya kununulia hekima ikiwa hana moyo wa ufahamu?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze maneno ya uzima kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Tusome maandiko ili tupate maana iliyo bora, rahisi na yenye kueleweka.

Mithali 17:16 “Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?”.

Hili andiko linamaanisha kuwa ni ile Hali ya mtu kuwa na uhitaji wa kupata hekima ndani yake kwa gharama yeyote ile lakini moyo wa huyo mtu unakuwa haupo tayari kuipokea hiyo heshima anayoihitaji ambapo hupelekea kupoteza muda na pesa kwa kulisumbukia jambo ambalo mtu anakuwa hana utayari nalo.

Hekima inayozungumziwa hapa siyo hekima ya Mungu bali ni hekima ya dunia ambayo ndiyo huwa inanunuliwa kwa fedha ili kumuwezesha mtu kupata maarifa yatakayo msaidia katika eneo ambalo mtu huyo anaona kabisa hakuna njia ya kuyapata hayo maarifa isipokuwa ni kwa kuyalipia na kusoma. Kwa mfano mtu anapoenda shule au chuo kusoma ili apate hekima itakayojibu maswali aliyonayo.

Katika hili neno tunaona pia kwamba kuna wakati mtu anaweza kutamani kufanya jambo Fulani lakini siyo kupenda kufanya jambo Fulani analolihitaji tena kwa moyo hii hupelekea kupoteza muda,fedha, kukata tamaa, kujidharau pia kuona Kila jambo ni gumu hata kama ni rahisi.

Funzo tunalolipata hapa ni kwamba tunapaswa kuitenda kazi ya Mungu kwa kumaanisha, kujitoa, na kwa kudhamiria toka mioyo yetu ili tuone matokeo yaliyo Bora na mazuri zaidi. pia tusipojitoa kwa moyo tutakosa muelekeo hivyo inatupasa kuwa na moyo wa kufanya vitu unavyovipenda toka rohoni ili tuone kesho.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *