Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Ili tuweze kuuelewa mstari huu vizuri tuchukulie mfano wa kuku anakwenda kuchinjwa baada hata ya dakika 20 au 10 huyo kuku mauti inakuwa inafanya kazi ndani yake. Maana muda si mrefu anakwenda kuchinjwa.
Lakini kwetu sisi ambao tunamla kuku uzima unakuwa unafanya kazi ndani yetu maana muda si mrefu tutakwenda kumla na tutapata afya njema ya miili yetu.
Kama maandiko yanavyosema..
2 Wakorintho 4:12 “Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu”.
Maandiko yanaanza kumzunggumzia Mwokozi wetu Yesu Kristo kama kondoo aendae machinjioni ambae ndio mwamba na mkuu wa uzima huu tulionao katika Yeye.
Isaya 53:7 “Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake”.
Sasa Bwana Yesu mauti ilimpata pale msalabani Kalvari sisi tumepata uzima ndani yetu tukimwamini yeye. Maana pasipo Yssu Kristo hakuna wokovu ambao sisi tungeliupata.
Maandiko yanaendelea kusema..
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Sasa sisi Wakristo tunapofanya kazi ya injili wakati wa mateso ili watu wengine waokoke Tafsiri yake kwetu sisi Mauti inakuwa inatawala lakini kwa watu wale tunaowapelekea injili uzima ndani yao. Maandiko yanasema..
Warumi 8:36 “Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa”.
Hivyo kwa kila mmoja mmoja aliekoka hatuna budi kujitoa kikamilifu katika kuifanya kazi ya Mungu. Kwa kukubali kufa kwa ajili ya wengine kudharauliwa, kudhihakiwa nk ili wengine pia wapate neema kama tuliopewa sisi kwa kuwa wana wa Mungu alie hai.
Tunapotoa uhai wetu(kwenda kuwahubiria) kwa ajili ya wengine sawa sawa na Kristo alivyojitoa kwa wengine ni kitu ambacho Kristo anakitazama kwetu sana. Na ni kitu kina baraka kubwa sana sana tunapokifanya..
Maana tunakuwa kama yeye.
1 Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu”.
Hivyo na sisi imetupasa kufanya hivyo hivyo kama mwokozi wetu alivyofanya..
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.