
NAYE MWENYE MOYO MKUU MIONGONI MWA MASHUJAA ATAKIMBIA UCHI SIKU ILE.
Amosi 2:13 “Tazameni, nitawalemea ninyi, Kama gari lilemeavyo lililojaa miganda.
[14]Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio; Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake; Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;
[15]Wala apindaye upinde hatasimama; Wala aliye mwepesi wa miguu hataokoka; Wala apandaye farasi hatajiokoa nafsi yake;
[16]Naye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa Atakimbia uchi siku ile, asema BWANA.
Ndugu usitamani kabisa siku ile ikukute (siku ya hasira ya Bwana), hebu fikiria kama mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa atakimbia uchi siku ile!, wewe mtu wa kawaida utawezaje kusimama siku hiyo?
Unaweza ukasema fedha zako sitakusaidia Lakini biblia inasema..
“Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha”.(Sefania 1:18)
Ndugu yangu, siku ile hakuna mtu atakayeweza kusimama mbele ya hasira ya Bwana, sio tajiri wala masikini, sio mkuu wala mdogo, siku hiyo hali za watu wote zitafafana. Sikia Neno la Mungu linavyosema..
Isaya 24:1 Tazama, BWANA ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.
[2]Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa hali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya bwana wake; kama ilivyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye; kama ilivyo hali yake atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaye faida.
[3]Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana BWANA amenena neno hilo.
Umeona hapo!! ogopa sana ndugu, leo hii matajiri na wafalme wa dunia hii wanajiona hakuna mtu wa kuwaambia kitu. Lakini siku ile watakimbia na kujificha chini ya miamba.
Ufunuo 6:12 Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
[13]na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
[14]Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
[15]Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
[16]wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
[17]Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye NI NANI AWEZAYE KUSIMAMA?
Siku ya Bwana inatisha ndugu, sio ya kutamani kabisa..ni mambo makuu na ya ajabu yanakuja kuikumba hii dunia.
Amosi 5:18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwani kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru.
[19]Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
[20]Je! Siku ya BWANA haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.
Unapoendelea kuishi katika dhambi, na huku unasikia injili ya msalaba Kila siku na hutaki kugeuka na kuacha maovu yako maana yake UNAITAMANI siku ile ya Bwana, lakini pia unatamani jehanumu ya moto.
Basi, kama leo utaisikia sauti ya Mungu na kuamua kumgeukia Bwana Yesu akuoshe dhambi zako utakuwa umefanya maamuzi ya busara sana na kamwe hautakuja kujutia.
Lakini kama bado utaendelea kufanya moyo wako kuwa mgumu na ukaendelea kuishi maisha ya dhambi.. ulevi, uzinzi, ukahaba, utazamaji wa pornography, kujichua/masturbation, usagaji, ulawiti, usengenyaji, rushwa, uongo, uvaaji mbaya (suruali, vimini, nguo za kubana), kuweka manywele bandia kwenye kichwa chako, kusuka, kupaka kucha rangi, kutumia mikorogo/makeup, kutoboa masikio na kuweka mahereni, na kutumia mapambo aina yoyote, kubeti/kamari, kucheza magemu, pamoja na mambo yote yasiyo na utukufu kwa Mungu na huku unajitumainisha na watu wengi ulionao nataka nikuambie siku ile utakuwa peke yako. Hautakuwa na mchungaji wako anayekudanganya kwamba Mungu anaangalia roho haangalii mwili utakuwa peke yako.
Kumbuka siku hiyo imekaribia sana kuliko unavyodhania. Parapanda italia muda wowote na watakatifu watanyakuliwa kisha dhiki kuu itaanza na hiyo siku kuu ya Bwana. Ni heri leo ukamkimbilia Yesu kwa kumaanisha kutubu na kuacha njia zako mbaya.

Ikiwa upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo na unahitaji msaada basi wasiliana nasi kupitia namba uzionazo chini ya makala hii nasi tutakusaidia bure kabisa.
Maran atha (Bwana Yesu anarudi)
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.