Neno vuruvuru linamaanisha nini katika biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Neno hili linamaanisha kuwa ni Hali ya vitu kutokukaa katika mpangilio mzuri ambao haudhihirishi muonekano sahihi wa vitu au jambo.

Turejee maandiko kama yalivyoelezewa na Bwana wetu Yesu Kristo ili tupate umeelewa zaidi utakaotupatia maana sahihi ya Neno hili

Isaya 17:13 “Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.

14 Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang’anya mali zetu”.

Tunaona jinsi ambavyo Mungu alivyowahakikishia kuwa ulinzi madhubuti upo na kwamba shetani hataki tujifunze zaidiili fahamu zetu zisifunguka.

Tunaona Mungu anasema kuwa atawakemea hao maadui wanaowafuata

Pia tunaona Bwana anasema kuwa watakuwa kama makapi mbele ya upepo hii inamaanisha kuwa maadui wote wanainuka na kuleta vita kwa Wana wa Mungu wataharibiwa na Bwana Mungu kwa kuwa neno la Bwana linasema kuwa Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu ambaye hawezi ruhusu maadui wawaharibu watoto wake na kama akiruhusu basi ufahamu kuwa anasababu za msingi za kuruhusu adui akupe wakati mgumu kama ilivyo kuwa kwa mtumishi wa Mungu Ayubu Bwana Mungu alisema.

Ayubu 2:6-8

[6]BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake.

[7]Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.

[8]Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni.

Pia Bwana aliposema kuwa watakuwa vuruvuru alimaanisha kuwa ataweka Hali ya kutokuelewana kati ya hao kiasi cha kuwepo kwa malumbano kati yao ambayo mwisho wa siku yangezalisha ugomvi usio na mwisho na hata kupelekea Kila mmoja kuwa na ratiba zake tu pasipo kurejeana kama kundi.

Hivyo Yesu Kristo anatufundisha kuwa tunapokuwa ndani yake yeye anapigana na majeshi ya Pepo wa baya, wachawi, nguvu za Giza na vyote vinavyotumwa kwetu kuleta uharibifu kama neno linavyosemwa kuwa vita si vyetu bali vita ni vya Bwana hivyo haitupasi kuogopa bali tuwe na ujasiri huku tukiendelea kumtumikia Mungu kwa furaha na kwa kuomba, kufunga, kusoma neno la Mungu, kulitafakari na kuliishi kama neno linavyosemwa kutoka katika.

Waefeso 6:10-13

[10]Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

[11]Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

[13]Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *