Shalom, Karibu tujifunze Neno la Mungu..
Kuzimu ni sehemu mbaya sana na yenye mateso makali yasiyoelezeka, ni mangojeo ya wale wote waliokufa kwenye dhambi, waliomkataa Bwana Yesu mioyo mwao, sasa wakifa ndipo wanapelekwa kuzimu, ni mahali ambapo hutamani hata adui yako awepo huko kwa hayo mateso yake..
Tunasoma hapa,
Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;
44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum;
[ 46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”.
Umeona hapo, ni heri ukapoteza hata kiungo chako kimoja lakini usiingie kuzimu, kwasababu kuna majuto makubwa yasiyo kuwa na msaada wala kusikilizwa, na baada ya hapo,siku ile ya mwisho utatoka kuzimu ili ukatupwe kwenye ziwa la moto,na huko maandiko yanasema ni kilio na kusaga meno, si mahali pakutamani kabisa..
Maisha yako yana uthamani sana, jiulize ndugu ukifa leo Katika hali hiyo uliyo nayo, utakwenda wapi?, utakuwa mgeni wa nani huko unakokwenda, umekuwa mtu wa kutenda dambi na kufanya maovu, injili umekuwa ukisikia inayokukemea kuacha dhambi lakini unaipuuzia, maandiko yanasema kuzimu haishibi watu wala haijai,
Mfano wa Mambo hayo tunayaona kwenye habari ya tajiri na lazaro, jinsi mmoja alivyopokea mema ambaye ni lazaro na mwingine mateso, yule tajiri akatamani hata tone la maji, lakini haikuwezekana, akatamani hata ndugu zake wasifike huko aliko lakini pia ilishindikana..
Embu soma hapa kwa umakini…
Luka 16:19-24,26,28-30
[19]Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
[20]Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
[21]naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
[22]Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
[23]Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
[24]Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
[26]Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
[28]kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
[29]Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
[30]Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
Umeona hapo, unapata wapi ujasiri wa kuchezea hatma ya maisha yako, nafasi unayo ya kutengeneza sasa, ni wewe kuamua kumpokea Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wako, na kisha kubatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo,ili upokee Roho Mtakatifu akuongoze kwenye Wokovu hata siku ya mwisho..
Ikiwa utahitaji msaada wa kumpokea Bwana Yesu wasiliana nasi kwa namba unazoziona mwisho wa somo hili, tukusaidie Katika hilo,
Na ikiwa uliokoka jitenge na mambo yote maovu, dhambi, ishi maisha yanampendeza Mungu,kwa kusikia sauti ya neno lake, kuwa mtu wa kusoma maandiko, kuomba na kuwahubiria wengine,na Bwana atakuwa pamoja na wewe..
Bwana akubariki..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.