Fahamu kwa nini Bwana aliwapofusha watu macho na kuifanya mizito mioyo yao?

Biblia kwa kina No Comments

 

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tujifunze maneno ya uzima ya mwokozi wetu.

Umewahi kujiuliza kwa nini Bwana aliwapofusha macho na kuifanya mizito mioyo yao ili wasiongoke/kumgeukia yeye? Je! Bwana anaetaka watu waokolewe kwa nini afanye jambo kama hili? Je hapendi watu waokolewe?Yapo maswali mengi sana unaweza kujiuliza juu ya jambo hili.

Lakini ipo siri kubwa sana hapa imejificha nyuma yake ambayo inatuhusu pia mimi na wewe Kristo anatamani tuifahamu.

Sasa hebu tuusome mstari wenyewe..

Yohana 12

39 Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena,

40 Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

Bwana Yesu ananukuu mstari huu kutoka katika kitabu cha nabii Isaya.(Isaya 6:10). Na aliokuwa akiwaongelea hapo ni wana wa Israeli(Baadhi yao wakiwemo Mafarisayo,Waandishi,Makuhani nk)ambao hawakutaka kuijua kweli/kuikubali kweli ijapokuwa walijua ukweli mioyoni mwao.

Sasa ni kwa nini iwe hivi?

Ni lazima iko sababu nyuma ya jambo hili.. kwa msaada wa Roho Mtakatifu tutaifahamu.

SASA NI KWA NINI?

kama nilivyosema hapo mistari ya juu kidogo kuwa Yesu alinukuu mstari huo katika kitabu cha Isaya na alikuwa akizungumza hapo na makutano Lakini kulikuwepo na Mafarisayo,Makuhani, na waandishi. Ambao waliufahamu ukweli na dhamiri zao zikiwashuhudia kabisa kuwa yote aliyokuwa akiyanena Kristo ni ya kweli. Lakini wakakataa kutii na kujifanya kana kwamba hawajaelewa kitu..

Waliufahamu ukweli kabisa wakajua kuwa kweli Yesu Kristo ametumwa na Mungu yaani ndio(Masihi)mwenyewe aliyenenwa na manabii hapo kale.. lakini wao kwa kuifahamu kweli wakakataa kuitii kweli na kubadilika na kumfata Kristo hilo tunalidhibitisha katika…

Yohana 3 1 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.

2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.

Unaona hapo! Huyu Nikodemo ambae alikuwa ni mkuu wa Wayahudi na Ni mmoja wa wakuu wa Mafarisayo alijua kabisa kuwa Yesu Kristo ndio Masihi. Ndio maana akamwendea usiku akitaka kufahamu zaidi na atii katika kile Kristo anachokifundisha.

Nikodemo hakuwa anafanya unafiki hapa maana Yesu angelimwambia hapo hapo kuwa yeye ni mnafiki lakini Yesu aliona nia Ya kweli iliyokuwa kwake.

Sio Nikodemo tu lakini katika baadhi ya wengi wa wakuuu nao walimwamino Yesu Kristo ndio Masihi Mwenyewe tunalidhibitisha hilo tena..

Yohana 12

42 Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.

43 Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.

Unaona hapo maandiko yanasema “…walikuwamo wengi waliomwamini;….”

Lakini waliogopa kujidhirisha/kukiri imani yao katika Kristo kuwa ndiye mwana wa Mungu kwa sababu ya kutengwa na Mafarisayo/Sinagogi.

Na mwisho wa siku baada ya kuzidi kukataa ukweli wakajikuta wanajawa na wivu,hasira nk wakapanga mipango ya kumuuwa Masihi.

Sasa Mungu aliachilia nguvu ya upotevu katika akili zao na Fahamu zao waone kabisa huyo sio Masihi na mwisho wamuuwe kabisa kwa sababu ya kuikataa kweli.

TUNAJIFUNZA NINI ?

Sasa maandiko yanasema..

2 Wathesalonike 2

10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.

11  Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.

Siri anayotaka tuifahamu Kristo iko hapo katika mistari hiyo na jibu la maswali yote ambayo tumeanza kujiuliza katika Mistari hiyo.

Unaona sababu ya hao Mafarisayo kupotea na kupelekea kumuua Kristo ni kwa sababu HAWAKUKUBALI KUIPENDA KWELI,WAPATE KUOKOLEWA.

Ndugu yangu leo hii kama hutakubali kuipenda kweli haijalishi unaomba sana,unatoa sana sadaka,unafunga sana,unanena kwa Lugha sana,unaweza kuichambua Biblia mwanzo mwisho. Lakini kama hutakubali kuipenda kweli ni kazi ya kuchosha..

Sasa kuipenda kweli kwa namna gani?

Unapohubiriwa/kusikia injili ikikuonya uache dhambi,ujistiri mwili wako,usirihribu hekalu la Roho Mtakatifu yaani mwili wako kwa kuuvalisha cheni,kuupaka wanja,Lipstick, kuvaa suruali,kuvaa mawigi.,vimini,vitop nk

ukiambiwa hivyo unakuwa mkali unakasirika na  unasema “TUMEOKOLEWA KWA NEEMA MUNGU HAANGALII MWILI” unaendelea kujitumainisha kwa vifungu vya biblia kwa kusema..”HUWEZI UKAPOTEZA WOKOVU KWA KUFANYA HIVYO TU MUNGU HAKUFANYA KAZI DHAIFU HIVYO NIPOTEZE WOKOVU KWA SABABU YA HIVYO TU HAIWEZEKANI nk”

Nataka nikwambie ndugu unajitumainisha katika uongo na mwisho wa siku unavyoambiwa na unaendelea kupinga ingawa hata Roho Mtakatifu anakushuhudia kuwa si sawa unaendelea kulazimishia unawaangalia waimbaji wa nyimbo za injili wa nyakati hizi unasema mbona wale wanavaa vile na vile hata mimi nikiwa kama wao Mungu hawezi fanya chochote ni wakati wa neema huu..

ndugu yangu neema haijaja kuhalalisha uovu kabisa..

Hivyo unavyoendelea kupinga mwisho wa siku Mungu anaachilia nguvu ya upotevu uendelee kujitumainisha katika hayo mwisho wa siku uangamie na nguvu ya upotevu ikishaachiliwa juu yako hutaweza kugeuka tena na utaona ni sahihi kabisa utaendelea kuona maono ya kweli kabisa kutoa unabii wa kweli kabisa, kufundisha na watu wakapokea na kuponya wagonjwa na hata kufufua wafu lakini tayari uko upotevuni.

Ndugu yangu kumbuka hili na litafakari sana “HATA MKE WA LUTU ALIPOTEZA WOKOVU KWA KITENDO CHA KUGEUKA NYUMA TU” akawa nguzo ya chumvi..

Neno la Mungu ni hai hivyo ni lazima litakuchoma,litakutafakarisha,litakupa kugeuka.. lakini jukumu la kugeuka ni lako sio la Mungu.  Ukiamua kumtii Mungu itakuwa heri kwako.

Hakuna faida yoyote katika hayo yote unayoyafanya na kupambana kuwa nayo mwisho itakuwa ni majuto kwako.

Itakuwa heri kwako kama umedhamiria kwenda Mbinguni ukageuka leo..

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *