Bwana Yesu Asifiwe.
Jibu: habari hii utaipata katika matendo 15..
Matendo 15:37 ″Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao.
38 Bali Paulo HAKUONA VEMA kumchukua huyo aliyewaacha huko pamfilia,asiende nao kazini.
39 Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana….”
Tukianzia sura ya 13:13 utaona Yohana hakuwa radhi kuongozana na Paulo na Barnaba kwa kuogopa dhiki ambayo huenda ingaliwakuta mbeleni katika Huduma (kupeleka injili katika mataifa). Lakini baada ya muda anakutana nao [ Paulo na Barnaba] na anaomba kujumuika nao Tena, jambo ambalo linapingwa na Paulo mtume, kwa maana tangu mwanzo Alishindwa kuambatana katika Huduma hiyo kwa sababu aliogopa taabu ambazo huenda zingewakumba hapo awali.
Kuhusu Msamaha, Paulo alimsamehe lakini hakuwa radhi kuambatana nae katika Huduma, maana huenda angekuwa kikwazo mbeleni katika kazi ya injili kwa Mataifa.
Habari hii ni Funzo kwa watumishi wa Mungu Katika injili, tusiambatane na Watu sababu ya urafiki bali tuangalie wale walio waaminifu.
Tusome..
Wafilipi 2:12 “…utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu”
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.