Ni sawa Mkristo kupokea pesa kutoka kwa mtu anayefanya kazi haramu?

Maswali ya Biblia No Comments

Jibu :Hairuhusiwi kupokea pesa kutoka  kwa mtu wa namna hiyo kwa kuwa katika ulimwengu wa Roho inaonekana na kuthibitika kuwa umeshiriki kufanya kazi haramu iliyopelekea kupata hicho kiasi cha pesa.

Tunaweza kurejea maneno ya uzima ambayo yatatupatia mwangaza juu ya hii ibada.

Luka 6:43 “Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri;

44 kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu”

Haitakiwi hususani katika masuala ya Mungu ikiwemo kuendelea huduma ya Kristo ikiwemo ujenzi wa kanisa n.k ikiwa kama anafanya kazi haramu itampasa huyo mtu ageuke na kumfuata Kristo na kuacha kazi haramu na kufanya kazi zenye utukufu wa Mungu ili hizo pesa zipokelewe na zipate kibali kwa Yesu Kristo.

Neno la Bwana linasema

Mithali 15:8 “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake”.

Inatupasa kutenda kazi zenye utukufu wa Bwana ambazo hazitatufunga kumtumikia Mungu.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *