Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.. Karibu tujifunze maneno ya uzima.
Katika nyakati za Mwisho hizi kuna mafundisho ya aina nyingi sana. Lakini si mafundisho yote yanamfaa mwamini ijapokuwa yanasemwa madhabahuni na watumishi wengi Lakini si mafundisho anayotakiwa kufundishwa mwamini.
Yapo mafundisho ya watu wanaotaka kufanana na Yesu na matamanio yao ni kwenda Mbinguni.
Lakini yapo pia mafundisho ambayo si ya watu wanaotaka kufanana na Yesu Kristo na hawana nia ama maono ya kwenda Mbinguni.
Haya ni mafundisho mawili tofauti.. hapa ni mahali pa kuwa makini sana wewe kama mwamini kama mtu mwenye maono ya kwenda Mbinguni.
Hivyo si kila fundisho linamfaa (linakufaa)mwamini la! Ni muhimu sana kujifunza kuchagua mafundisho ambayo ni sahihi.
Leo tutaangalia aina ya mafundisho machache yanayomfaa mwamini na yasiyomfaa mwamini.
Mafundishoyanayomfaa mwamini.
1.Utakatifu & Ukamilifu.
Fundisho hili ni muhimu kwa mtu mwenye dhumuni la kwenda Mbinguni ni lazima afundishwe na aliishi pia.
Ipo tofauti kubwa sana hapa na watu wengi hawafahamu wengi tunajua tunapookolewa tunaitwa watakatifu na ndivyo ilivyo kweli tunaitwa watakatifu. Lakini tunaweza tunaweza kuitwa watakatifu na bado tukawa ni wezi, waongo,wasingiziaji,watukanaji,wenye hasira,tusiosamehe,wenye visasi,wivu,husuda,tunaangalia picha za ngono na kutwa nzima tunashinda tunaangalia tamthilia za kidunia zenye maudhui ya uzinzi na ulipizaji visasi na ushoga nk.
Yaani ni kwamba unaweza ukaitwa Mtakatifu na hauuishi au huendani kabisa na utakatifu au na hilo jina.
Kama mwamini Fundisho sahihi la msingi sana linalokuhusu ni utakatifu yaani kuyaishi maisha matakatifu na unavyozidi kuyaishi maisha matakatifu ndio unavyozidi kupanda ngazi za Ukamilifu.
Ambazo Mtume Petro amezisema vyema ambazo ziko saba ambazo kila Mkristo anatakiwa kuzipanda.
2 Petro 1
5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,
6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,
7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.
10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.
Unaona hapo mstari wa tisa(9) anasema.. “YEYE ASIYEKUWA NA HAYO NI KIPOFU HAWEZI KUONA VITU VILIVYO MBALI…”
unaona kwamba Mkristo asiekuwa na haya mambo maana yake ni kipofu na hawezi kuona vitu vilivyo mbali kwa namna gani? Maandiko yanasema.
Wakolosai 3:2“Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.”
Maana yake Mkristo huyu hataweza kabisa kuyatafakari yaliyo juu maana atakuwa ni Mkristo lakini anaewaza mambo ya mwilini ambayo tutayatazama baadae. Na maandiko yanaendelea kusema sisi wenyenji wetu(mwamini) ni mbinguni hapa hatuna budi kuishi kama wageni tu tena tusiokuwa na muda mrefu tukitazamia kwenda kwetu.
Hivyo fundisho la mwamini linafaa kuegemea sana katika kufika ng’ambo kule.. sio katika mambo ya ulimwengu huu.
2. Upendano(Upendo)
Kama mwamini ni fundisho ambalo linakufaa sana kila siku kupiga hatua katika upendo.. si upendo kama wa watu wa kidunia walio nao la!
Upo upendo ambao watu wa ulimwengu huu hawawezi kuwanao huo unazalishwa ndani ya mtu aliemuamini kweli kweli Yesu Kristo.
Upendo huo ni wa wewe kuwapenda adui zako na kuwaombea.(yaani hata mtu aliekuchukulia mume. Mke nk huyo mtu hutakiwi kumchukia wala kumtukana bali inabidi Umpende na umuombee sio kwa dakika moja hata Lisaa limoja kiwango cha chini mpaka mawili nk).
Mathayo 5
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
Kuwapenda wengine na kuwaombea zaidi hata ya unavyojiombea wewe na kujipenda wewe.. kujitoa kwa ajili ya wengine(kama Bwana Yesu).
Kutokuwa mtu wa Mwilini nk haya ni baadhi ya mambo machache tu ambayo unatakiwa kuwa nayo wewe kama mwamini au mafundisho unayotakiwa kufundishwa ni lazima yaegemee huku sana katika kukujenga na kukutengeneza ili Mwisho wa siku ufanane kweli kweli na Yesu Kristo).
Kukemea dhambi.. dhambi haina urafiki kabisa na mtu anaeitwa Mtakatifu hata siku moja.. nia ya dhambi ni mauti siku zote..(Warumi 6:23)inadai uhai wa mtu aende katika ziwa la moto hivyo mwamini Fundisho hili ni muhimu sana na ni sahihi maana litakufanya utambue na kuelewa madhara ya dhambi na dhambi ni kitu gani na kwa nini uiepuke na inataka nini kwako? Na bado inakuweka mbali na uso wa Bwana(inakutenga mbali na Bwana kabisa inakutumikisha kufanya usiyotaka nk).
Ukiona mambo haya hayafundishwi mahali hapo ulipo jiulize mara mbili mbili.
Mafundisho yasiyomfaa mwamini.
Hapa pia tutaangalia machache.. haya ni mafundisho ambayo hayana kabisa umuhimu kwako na yanalenga sana kukutumainisha katika mambo ya ulimwengu huu..
1.Mafanikio ya mwilini.
Si kwamba haya mafundisho ni mabaya au kwamba Mungu hataki tufanikiwe katika mwili la! Kristo anataka sana pia tufanikiwe katika mwili na sio dhambi kufanikiwa katika mambo ya mwilini kama vile Fedha,biashara nk.
Lakini hiki sio kiini au fundisho ambalo ndio linatakiwa liwe msingi kwako wewe kama mwamini hili ni ziada tu.. hata usipofundishwa Bwana atakupa tu maana unastahili kupata.
Lakini ukiona kila siku au fundisho unalolipokea asilimia kubwa limeegema kwenye mambo ya namna ya kufanikiwa kibiashara na kupata fedha, majumba nk kila siku unatiwa moyo na kupewa mbinu tena kutoka kwenye biblia(Biblia ni kitabu kinachoweza kukusapoti kwa fundisho lolote lile hata ukitaka ufundishe uzinzi na uone ni sawa biblia itakudhibitishia ni sahihi lakini la sio dhumuni kabisa hilo.)
Kila mchungaji akipanda ni mambo ya mafanikio tu unagusiwa kidogo sana mambo ya Roho Mtakatifu nk. Unaaambiwa “Yesu anakwenda kuinua biashara yako.. usikate tamaa hilo ni jaribu lako, wote walioshikilia biashara yako wanakwenda kuangamia, pokea mume pokea gari nk).
Wala huskii unakwemewa dhambi,ukiingia kuomba unaambiwa ombea biashara yako wala sio ujazwe Roho Mtakatifu.
2.Mafundisho ya ukombozi..
Kila siku unakwenda kukomboa ardhi,mzao wa kwanza,kila siku unakwenda kufunguliwa vifungo.. ndugu tangu siku uliyoamini umeshakombolewa tayari..wala hakuna laana yoyote uliyonayo wala mikosi nk ni kwa sababu ya kukosa ufahamu na maarifa unadanganywa na kwakuwa ni mvivu wa kujifunza.
Unafundishwa mafundisho miaka nenda rudi ya uzima wa milele unaambiwa huwezi upoteza umeshaokolewa umeokolewa milele na ishi utakavyo ndugu haya ni mafundisho ya watu waliokata tamaa na wamekubali kujisalimisha kwenye dhambi wameona kuwa dhambi haiwezekani kuishinda kwao yaani kuishi maisha matakatifu haiwezekani wakati inawezekana kabisa(Mathayo 5:48).
Na Wakristo wa namna hii hawayatafakari yaliyo ya juu bali ya chini tu basi.. ukiwambia kuishi maisha matakatifu wanakwambia ndio nini? Yesu watakwambia Yesu kashalipa kila kitu(ni kweli lakini Yesu Kristo hawi radhi na wapumbavu. Katupa Roho wake Mtakatifu ili atusaidie kuenenda sawa sawa)
Ni watu wasiokuwa na kiasi na ni mafundisho yanayokufanya usiwe na kiasi uishi kama watu walioko gizani tu sababu ni kwakuwa huwezi poteza uzima wa milele.. na mafundisho haya yanawashika watu wengi sana wanajiepusha na kusikia ile kweli kama maandiko yanavyosema..
2 Timotheo 4.
3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
5 Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.
Mafundisho yanayohusu shududa za watu walioenda kuzimu na kurudi na mambo ya uchawi(ambayo kwa asilimia kubwa yanakutisha tu) hayana maana kabisa kwako.
Mafundisho ya kuwaombea adui wako waanguke (ambao ni binadamu wenzako kabisa.) Na wakati neno linasema waombee wewe unaweka kwenye pipa la Moto wateketee ndugu sivyo.
Hivyo hayo ni baadhi ya Mafundisho ambayo hayatakiwi kuwa ndio msingi wa mtu anaetaka kwenda katika mbingu mpya na nchi mpya,utawala wa miaka 1000 au kwenda kwenye karamu ya mwanakondoo haya Mafundisho si sahihi kwako.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.