Nini maana neno alani?(1Samweli 17:51)

Maswali ya Biblia No Comments

Alani ni mfuko unaovaliwa kiunoni na askari kwa ajili ya kuhifadhi upanga hasa wakati wa vita….

Neno hili tunaliona katika vifungu vifuatavyo….

1Samweli 17: 51 “Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia”

1Nyakati 21:27 “Bwana naye akamwamuru malaika; naye akaurudisha upanga wake alani mwake tena”.

Yohana 18:11 “Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?”

Soma pia, Ezekieli 21:3:5

Tunapata mafunuo gani kiroho kuhusu Alani?


Sote tunafahamu huwezi kutenganisha upanga na alani kama tu ilivyo kwa pesa na pochi. Neno la Mungu ndilo upanga (Waefeso 6:17, Waebrania 4:12). Na moyo wa mtu ndio unaohifadhi neno la Mungu,

linapotakiwa kutumika hutolewa moyoni wala hakuna sehemu nyingne utalitoa, hivyo basi alani inafananishwa na moyo na upanga ni neno la Mungu…

Upanga unaweza kutumiwa na mtu yoyote na wakati mwingine humdhuru hata yule anayeumiliki, ndicho kilichotokea wakati shetani akimjaribu Yesu nyikani, alikuwa akimwambia ‘imeandikwa’ hakujua kuwa Yesu aliushika vizuri upanga wa neno kwa sababu aliijua ‘kwel yote’jambo lililompa ushindi dhidi ya shetani.

Mpendwa ni muhimu kuijua na kuijaza kweli yote ya neno la Mungu ndani ya mioyo yetu. Neno peke yake halitoshi bali tunaihitaji ile kweli ya neno la Mungu.

Kuna wakati shetani hulitumia neno kuwaangusha watu, anaweza kukwambia kuoa mke zaidi ya mmoja si vibaya tena anakupa na mifano ya watu kama Yakobo, Daudi, Sulemani ambao walifanya hivyo na bado Mungu aliwakubali hata wewe ukioa wake wengi haina shida. Swali la kujiuliza ni je hii ndiyo kweli yote ya neno la Mungu? bila shaka hapana, kweli yote ya neno la Mungu inasema Mungu alimuumba mtu mume na mke na hao wawili watakuwa mwili mmoja(Mathayo 19:4-9)kulikuwa na Adam mmoja na Hawa mmoja

Ni vyema kumuomba Roho Mtakatifu atusaidie kuyaelewa vizuri maandiko ili shetani asituangushe. Neno linatuambia tuivae kweli kiunoni.


Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,”

Ubarikiwe 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *