Neno hili tunapoliona katika maandiko lina maana mojawapo kati ya hizi tatu,
1.Kushiba kiasi cha kutotaka tena kile ulichokipokea awali
2.Kuwadharau watu wengine na kuwafanyia mambo ambayo hupaswi kuyafanya
3.Kujigamba /kujiinua na kudhani wewe unajitosheleza mwenyewe
Vifungu vifuatavyo limetumika kwa maana ya kushiba..
Mithali 27:7[7]Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.
Mithali 25:17[17]Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na kukuchukia.
Mhubiri 1:8[8]Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
2.Vifungu vifuatavyo vinaonyesha kukinai kama kudharau wengine kwa kukaidi maagizo kwa kukusudia.
Kumbukumbu la Torati 17:12[12]Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli.Soma pia…
3.Lakini pia sehemu nyingne tunaona kukinai ni kama kujihesabia haki mwenyewe..
Luka 18:9-14
[9]Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
[10]Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
[11]Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
[12]Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
[13]Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
[14]Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa…
Sisi hatutakiwi kuwa na sifa kama hizo, tunapoenda mbele za Mungu tusijihesabie haki tuwe wanyenyekevu watu wenye kuomba rehema mbele za Mungu kuliko kusema sifa zetu na Mungu atatukubali maana yeye huwapenda wanyenyekevu lakini huwapinga wenye kiburi.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.