Nini maana ya mstari huu kwenye waefeso Waefeso 5:16[16]mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana yesu apewe sifa mwana wa Mungu
Tushukuru Sana Kwa neema ya kuiona Leo maana si Kwa nguvu wala Kwa uweza Bali Kwa huruma,fadhili na mapenzi yake basi tuna paswa kujifunza neno lake kila tunapo muda na wakati maana lipo kusudi la Mungu kusoma huu ujumbe.

Waefeso 5:15-18 biblia inatuambia hivi.. “15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16 MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za uovu.

17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

Maandiko yanaposema kuukomboa wakati nini maana yake? Tutajifunza kwa undani zaidi Hapo Kwa haraka tafsiri rahisi ya hili neno kuukomboa wakati ni

kuutumia muda vizuri”,

tulipokuwa tuna soma moja ya vitu ambavyo vilikuwa vinawaudhi na kuwakasirisha sana walimu,ni pale walipokuwa wanaona wanafunzi wanautumia muda wao vibaya (hawaukomboi wakati), Hususani pale mwalimu anapotazama muda aliobakiwa nao ni jinsi gani ulivyo mchache, topics bado hazijaishaza za kusoma, halafu mwanafunzi, Hana muda kabisa wa kujisomeia anapiga kelele darasani, hazingatii masomo, haudhurii darasani,ana chelewa kwenye vipi na wakati mwingine anatoroka na kwenda kwenye Mambo mengine ya ajabu inawatia sana hasira waalimu pamoja na wazazi. Vivyo hivyo na katika mambo mengine.

Ila tukiangalia pia katika neno la mungu maandiko Yana tuagiza tuukomboe wakati, kwasababu biblia imeweka wazi kabisa kuwa sasa zamani hizi ni za UOVU, na huo wakati tuna ukomboaje sasa na kwa namna gani? Biblia inasema ni kwa kutaka kuyafanya kufahamu na kuya timiza yaliyo mapenzi ya Mungu kwetu.Huko ndiko kuukomboa wakati kuliko na maana mbele za Mungu.

Mpendwa sasa ulimwengu una mambo mengi na masumbufu mengi sana, Ni kweli tunafahamu kwa sehemu moja au nyingine hatuwezi kuepuka masumbufu namihangaiko kama ipo lakini tume pewa onyo tuishi kama watu wenye hekima, na sio wajinga, tukijua kuwa sisi ni wapitaji tu hapa duniani, na siku zetu zinakimbia kwa mbio sana, biblia inasema sisi ni kama MVUKE uonekanao kwa kitambo kisha kutoweka (Yakobo 4:14), Mvuke sio kama moshi ambao unaweza walau ukauona ukipaa mawinguni, mvuke wenyewe hata kwenye dari haufiki umeshapotea, ndivyo maisha yetu yalivyo. Biblia inasema na mwanadamu ni kama maua ambayo hayo hayana maisha marefu,

(Zaburi 103:15 ”Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo).

Hivyo Hata tukiishi miaka 70 tu au miaka 140 bado siku zetu zitabakia kuwa ni chache sana. Hivyo jambo tunalopaswa kujiuliza kama tutakufa leo huko tuendako ni jambo gani la maana litakalo onekana tumelifanya hapa duniani?. Kwasababu kule hatutaulizwa tulikuwa na majumba mangapi, au hela kiasigani au magari mangapi, au biashara ngapi, au watoto wangapi,wala hatutaulizwa tulikuwa maskini kiasi gani LA! Tutaulizwa ni kitu gani tumeongeza katika ufalme wa mbinguni..Tukiliweka hilo akilini basi itatusaidia sana kuishi kwa umakini.

Tunamwona Bwana wetu Yesu alijua nini maana ya kuukomboa wakati, angalia alichowaambia wanafunzi wake..

Yohana 9:4 ”Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi…”


1 Wakorintho 15:58
[58]Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.

Tunaona Japo alikuwa ni Mungu katika mwili alijua nini maana ya muda, kuwa kuna kipindi na wakati kinachoitwa usiku (KIFO) ambacho mtu yoyote atatamani kufanya kazi ya Mungu asiweze, Na tunamwona Bwana wetu japo aliishi miaka 33 tu lakini kazi aliyoifanya ina matunda makubwa mpaka sasa tunayafaidi. Hiyo ni kwasababu aliukomboa muda wake vizuri hapa duniani ipasavyo. Wakati mwingine hakuwa na muda hata wa kula. Alipoletewa chakula ili apate kuitimiza kazi.

NA SISI JE! TUNAWEZAJE KUUMBOA WAKATI WETU?

Jibu ni ndio tunaweza kuukomboa wakati kwa kuidhamini siku inapoanza tumwombe Mungu atusaidie tufanya jambo ambalo litakuwa na matunda katika ufalme wa mbinguni na katika maisha yetu ya rohoni tuziangalie siku zetu zikiwa zinaweza kupita siku , wiki, mwezi bila kuona kitu chochote cha maana tulichokifanya kwa ajili ya maisha yetu ya rohoni au kwa ajili ya ufalme wa Mungu, basi tujue hatuukomboi wakati haijalishi tunatengeneza mabilioni ya pesa kiasi gani kwa siku. Jamani huu ndio wakati wa kuanza kuitengeneza mambo yako upya mbele za Mungu, kabla ya siku ile kufika.

Muda ambao unautumia kuchati kwenye magroup ya whatsapp, au kusoma habari zisizokuwa na maana mitandaoni, na kuangalia vitu ambavyo avifai mitandaoni komboa wakati kwa kutumia muda huo kujifunza Neno la Mungu, au kusoma mahubiri au mafundisho ya Neno la Mungu. hayo ndio mapenzi ya Mungu kwako, au tumia muda huo kukaa katika utulivu kumsifu na kumwimbia Mungu wako..peke yako au pamoja na wakristo wengine..

Tukiwa makazini kwetu, kwenye biashara tumwombe Mungu atusaidie, sio wakati wote, tutakuwa buzy na shughuli, au kuongea na wafanyakazi wenzetu mambo ya kikazi, tutumie muda wetu wakati mwingine kuwashirikisha habari za Yesu kristo, huku tukiwaelekeza katika vyanzo vizuri vya kupata habari za Mungu, kwa kufanya hivyo pia tutakuwa tumeukomboa wakati na siku yetu kuwa na maana mbele za Mungu.

Muda ambao tumekaa hatuna shughuli yoyote, tunaweza tumia muda huo kwenda kuomba, hata kama hatutakuwa na mahitaji wakati huo mbele za Mungu, lakini pia tumeagizwa kuwaombea wengine, hivyo tumia muda huo kuwaombea watu wengine, kuna ndugu zako, rafiki zako, jamaa zako, taifa lako, kanisa n.k..Kwa kufanya hivyo utakuwa umeukomboa wakati. Na pia maombi yanasaidia kuepukana na majaribu.

ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *