Nini maana ya neno rubani kama lilivyotumika kwenye biblia (ezekieli 27:8)

Maswali ya Biblia No Comments

Pitia hapa..

Ezekieli 27:8 “Wakaao Sidoni na Arvadi ndio waliovuta makasia yako; wana wako wenye akili, Ee Tiro, walikuwa ndani yako, ndio WALIOKUWA RUBANI ZAKE”.


Marubani tunaowasoma hapo hawakuendesha ndege kama marubani wa sasa hivi kwa sababu kwa wakati huo ndege hazikuwepo. Neno rubani asili yake ni mwana maji na sio mwana anga kama linavyotumika sasa hivi,hivyo rubani katika biblia maana yake ni nahodha…

Siku hizi kumekuwa na mavumbuzi mengi na maneno mengi yamekuwa na maana zaidi ya moja, mfano Biblia ilipotaja magari (Mwanzo 45:21)ni magari lakini sio kama tuliyonayo sasa hivi, hata sehemu tunayoona risasi imetajwa (Kutoka 15:10)haikuwa risasi kama tunayoijua sasa hivi, lakini pia tunaona kuna ufisadi uliozungumziwa katika biblia ambao ni tofauti na huu ulipo sasa hivi (2Petro 2:7)

Hivyo Rubani aliyezungumziwa katika Ezekieli 27:8 ni rubani mwana-maji na si mwana-anga, unapoendelea kusoma mstari wa 29 maandiko yanaelezea vizuri


Ezekieli 27:29 “Na wote wavutao kasia, wana-maji, na RUBANI ZOTE WA BAHARINI, watashuka katika merikebu zao, na kusimama katika nchi kavu”.


Tunaona maandiko yanasema Rubani zote za Baharini maana yake ni mwana maji..


Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *