NINI MAANA YA YEYE ALIYE NA SIKIO NA ASIKIE

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom. Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Tukisoma katika kitabu cha ufunuo katika sehemu tofauti tofauti/sura neno hili limejirudia rudia zaidi ya mara 2.

Ufunuo wa Yohana 2:17 YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ASIKIE neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa……”

Lakini ukisoma tena..

Ufunuo wa Yohana 2 7 YEYE ALIYE NA SIKIO, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa…….

Mathayo 11:15

Pia tukisoma katika Mathayo..

Mwenye masikio, na asikie.Neno hili limejirudia mara nyingi zaidi katika maandiko.

Sasa je nini hasa maana ya neno hili? Ili tuelewe vizuri tusome..

Marko 8: 18“Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki?”..

Sasa ukisoma vizuri utaona Bwana Yesu hakuwa anaongea na viziwi au wapagani bali alikuwa anaongea na wanafunzi wake walioamua kujikana nafsi zao na kumfata yeye. 

Kusikia ambako alikuwa anapazungumzia Bwana Yesu katika sehemu zote hizo na nyingine ni kule kusikia kwa masiko ya ndani(ufahamu na uelewa juu ya ujumbe mahususi unaozungumziwa.)kwa maana nyingine tunaweza kusema ni uelewa sahihi wa mambo ya rohoni.

Hivyo hivyo na sisi tunaposoma maandiko hatutakiwi kutoka pale na stori fulani bali tunatakiwa kupata fundisho lililoko nyuma ya habari hiyo katika Roho Mtakatifu.yaani tunafunuliwa na Roho(ufunuo).

Hivyo tunapaswa tusikie sauti ya neno lake sio kuishia kuona maandishi peke yake tu.. kama jinsi maandiko yanavyosema..

Zaburi 103:20 Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake. 

Unaona  hapo? Anasema “….Mkisikiliza sauti ya neno lake” kumbe siku zote sauti ya neno lake ipo jukumu letu sisi ni kuisikiliza. Kama tutakuwa makini basi tutaisikia kabisa.

Mfano maandiko yanaposema “usimuzuie ng’ombe apurapo nafaka….” Sehemu nyingine maandiko yanasema “ng’ombe wa jirani yako ukimuona amepotea Sharti umrudishe…”nk hatupaswi kuanza kutafakari mambo ya ng’ombe hapo tena. Inabidi tutafakari na kupata ufunuo wake hapo. Tukijua fika hapo Mungu alikuwa haongelei ng’ombe bali alikuwa anazungumza na sisi kupitia kivuli/mfano wa Ng’ombe kutufikishia ujumbe sisi ni kwa namna gani tunapoona mwenzetu katika imani tunapoona anapotea katika imani tumrudishe kwa kufanya Juhudi ili kuhakikisha anarudi na si kumuangalia akienda kuangamia. Nk.

Hivyo na sisi tuwe ni watu ambao kila siku tunatafakari ili kupata ujumbe ambao Yesu amekusudia tuupate.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *