NINI UNACHOTAKIWA KUKIFAHAMU JUU YA NENO LA MUNGU?

Biblia kwa kina No Comments

Shalom nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.

kuna mambo ya muhimu sana kama mwamini unayotakiwa kuyaelewa ama kuyafahamu juu ya Neno la Mungu? Kama usipoelewa kuna hatua hutafika kamwe.

Kuna mambo mengi ya Msingi yanayokuhusu na ni kwa faida yako hutayafahamu na utaelendelea kuishi katika hali ya unyonge,udhaifu,kukata tamaa,leo una furaha kesho huna leo uko hivi kesho vile hali yako ya rohoni mpaka mwilini itakuwa haieleweki.

kwa sababu kama usipojua/kufahamu utakua unatembea kwa hisia zako,utafanya maamuzi kwa hisia zako, lakini sio katika uhalisia wa Neno la Mungu, Wakristo wengi wanatembea kwa hisia kuliko Imani ndio maana leo wanahisi au kuona vile kesho wanahisi na kuona kivingine leo wanaujasiri kesho hofu imetawala lakini ukikaa katika neon la Mungu ukafahamu juu ya kile ambacho Neno linasema nini na Neno ni kitu gani basi utaishi maisha ya ushindi siku zote katika maisha yako.

1.Usilitofautishe Neno la Mungu na Mungu mwenyewe.

Tatizo kubwa linaanzia hapa wakristo wengi wanalitofautisha Neno la Mungu na Mungu mwenyewe yaani wanaona Neno ni Neno na Mungu ni Mungu hivyo mtu anajikuta anasema anamuamini Mungu lakini anakuwa na mashaka na Neno la Mungu kitu ambacho si sawa.

fahamu kwamba Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe(Hili watu wengi wanalifahamu lakini sio katika ualisia wana head knowledge tu kwamba ni hivyo lakini walichonacho mioyoni mwao sio uhalisia wa kile wanachokisema).Ni sawa sawa na sisi tumekua tumekuta kuna namba moja inaandikwa 1 tukiulizwa kwa nini iandikwe hiyo kwa nini hata isiandikwe / hatujui ila tunajua hivyo tu basi. Tukiulizwa kwa nini ina itwa moja hatujui ila tunafahamu ni 1.

kivipi Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe? Ili kuelewa kwa urahisi jambo hili tafakakari huu mfano hapa.

Rafiki yako hajafanikiwa kufika kanisani jumapili na akakuuliza baadae baada yawewe kutoka kanisani akakuuliza huenda kwa njia ya simu au mkakutana kwamba jumapili kuna matangazo yapi na yapi baada ya ibada mlitangaziwa kuhusu vijana? Halafu umwambie hakuna tangazo ambalo lilikua linahusu vijana, na wakati kumbe mlitangaziwa vijana wote siku ya jumatano kutakua na mkesha halafu rafiki yako akaja kusikia jumapili kwamba jumatano ile kulikua na Mkesha wa vijana na wewe ulimwambia hakukua na ratiba yoyote inawahusu swali la kujiuliza ni hili.

je? Rafiki yako atasema maneno yako yamemdanganya au wewe ndio umemdanganya? Ni wazi atasema “ Fulani alinidanganya” hatasema “ maneno ya Fulani yamenidanganya” maana yake maneno yake ndio yeye mwenyewe.

maandiko yanasema Neno alifanyika mwili..

Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”

2. fahamu Neno la Mungu ni hai na lina nguvu.

Waebrania 4:12

Wakristo wengi wanalifahamu hili lakini sio katika uhalisia ndani ya mioyo yao kwanza lazima ufahamu Neno la Mungu ni hai kama mtu akiliamini lazima ataona matokeo tu.

Wakristo wengi wanaona Neno ni maadishi tu au maelekezo tu basi au ni mwongozo wa dini nk.

Wakristo wengi wanayapa nafasi kubwa mashaka kutawala ndani yao kuliko Neno, na ndio hapo mtu utakuta ana mistari mingi ya mafanikio,ya uponyaji lakini haina matokeo yoyote kwake kwa sababu ya mazingira ya nje hata kama anatamka anatamka tu lakini yeye mwenyewe hategemei kuona mabadiliko katika hicho.

ndugu yangu weka akilini hili unapotamka Neno tegemea mabadiliko na amini ni kweli, usizipe nafasi akili zako zilizo na mipaka zitakwambia hili haliwezekani lakini lipe nafasi Neno kwamba yote yanawezekana hakuna gumu. Neno linasema..

Marko 9:23” Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.”

ukisoma kuanzia juu kidogo utaona kisa ambacho ukikitafakari utaona uhalisia kamili wa wakristo jinsi ulivyo.

ng’ang’ana kuliamini Neno hofu na mashaka vinapokuja kata kwa sababu hivyo vyote vinakufanya usione uhalisia(kumbuka hofu sio hisia ni roho na maandiko yanasema hatukupewa roho ya hofu)

Yesu anasema…

Yohana 6:63” Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”

Yesu anasema “maneno hayo niliyowaambia ni roho tena ni uzima” hasemi maneno hayo ni mfano au ni hadithi la!

chukulia mfano mtu akikwambia maneno mazuri kuhusu wewe hata kama hayana uhalisia kwako unahisi nini na ndani yako unajionaje ni wazi yanaamsha kitu fulani ndani yako? Hata akikwambia maneno mabaya vivyo hivyo. Ikimaanisha maneno yamebeba kitu kikubwa sana.

sasa hayo ni maneno yetu vipi kuhusu Neno la Mungu.

3.Usilitilie mashaka Neno la Mungu amini.

anza kuifundisha akili yako kukubaliana na uhalisia wa Neno la Mungu kwa sababu kinachopingana na uhalisia wa  Neno la Mungu sio roho yako kwa sehemu kubwa ni akili yako, kwa sababu imeshakua affected na mazingira.

Unapolitilia Neno la Mungu mashaka ni unamtilia Mungu mwenyewe mashaka na ndio maana mara nyingi ukiwa una mwambia mtu na unaona haamini unachomwambia lazima utasema “ *Huniamini mimi* ” husemi huyaamini maneno yangu? Kwa sababu mtu akiamini maneno yako amekuamini wewe na maneno yako ndio uhalisia wako.

Mungu alionyesha uhalisia wake kupitia Yesu Kristo pale Neno alipofanyika mwili(Yohana 1:4)

4.Neno la Mungu ni kweli.

Amini ikiwa Mungu amesema kitu kitatimia tu kwa sababu kisipotimia hatuwezi kusema Neno la Mungu ni uongo tutasema Mungu ni Muongo. Na ndio maana yote anayosema ni uhalisia na ndio ukweli amini hivyo.

yapo mengi sana unayopaswa kuyafahamu lakini leo kwa uchache anza kuaweka akilini haya.
tumia Muda wako mwingi kusikiliza mafundisho ya neno la Mungu kwa watumishi wa Mungu maana imani chanzo chake ni kusikia (Warumi 10:17)omba baada ya kumaliza kusikiliza kiri kile neno linasema ju yako, jitamkie yote ambayo Neno linasema juu yako.

Usifanye kwa siku moja au mbili fanya hivyo kila siku ndani hata ya mwezi mzima tenga dakika 15 kuhusu jambo moja tu kukiri Neno. Utaona mabadiliko usiamini akili yako itkwambia haiwezekani,

kiri hata kama siku hiyo hauna mood.

ubarikiwe sana.
Maranatha
mawasiliano:0613079530
@Nuru ya upendo.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *