Shalom karibu katika kujifunza Neno la Mungu
Tutajifunze kwa mfano huu ambao ni wa kawaida tu katika maisha yetu ya kila siku, kwa mtu anayetumia kwa ajili mawasiliano, lakini huwa unafika mda, hawa watu wa mitandaoni, wana toa ofa kwa wateja wao
Lakini japo huwa wanatoa ofa, lakini huwa wanaweza mda wa mwisho kutumia ofa uliyopewa, hata kama ofa iwe kubwa au ndogo lazima tu mda wa mwisho wa matumizi utakuwepo tu, mda huo ukifika ikiwa umeitumia ofa yako au ujatumia wao hukata tu hawatazami kama umelitumia
Tunajifunza nini katika maisha yetu ya rohoni pia, siku tu tulipozaliwa tulipewa wakati wa kutumika hapa duniani na ndiyo maana utaona watu wanakufa, kwa sababu mda wao walipewa umeisha.
Mhubiri 3:1-2
[1]Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
[2]Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa;
Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
Ikiwa kama tutashindwa kuutumia mda vizuri tulipopewa tujue kabisa kuna wakati utafika, huo uhai utaondolewa sasa jiulize, huo wakati ukifa huo mda uliyopewa wa kukaaa hapa duniani umeutumia ipasavyo?
Na Mungu kutupa huu mda si kwa sababu anataka tuje tutalii bali dhumuni kuu lilikuwa ni kuyafanya yaliyo mapenzi yake, kumwakilisha yeye, kumtumikia yeye hiyo ndiyo jumla ya mambo yote
Mhubiri 12:13-14
[13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
[14]Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Hukupewa mda ujirushe na mambo ya ulimwengu huu, au ufatishe namna inavyofanya, bali jumla ya yote ni kumcha Mungu na kufata maagizo yake, kijana, Binti, mama, na baba huo si wakati wa kucheza, mda huu ulionao utumie vizuri kabla ujaondolewa na fahamu kabisa baada ya kifo ni hukumu, Leo hii basi jitahidi kuishi maisha ya kumcha Mungu, maana sisi ni wasafiri
Ubarikiwe..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.