TAZAMA MWANA-KONDOO WA MUNGU AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU.

Biblia kwa kina No Comments

TAZAMA MWANA-KONDOO WA MUNGU AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU.

Jina la Bwana na mwokozi wetu, Mkuu wa uzima, Mfalme wa wafalme, Yesu Kristo libarikiwe.

Leo tutaangalia ni kwa jinsi gani BWANA YESU alichukua dhambi ya ulimwengu kama Yohana Mbatizaji alivyomnena katika..

Yohana 1:29 “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”.

Je unafahamu kuwa kama si Yesu, habari yetu ingekuwa imeisha zamani sana!!

Biblia inasema..

Zaburi 14: 2 “Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja”.

Sehemu nyingine inasema..

”Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe;..” (Isaya 53:6)

Unaona! Sasa kama hakuna hata mmoja aliyeonekana duniani mwenye haki..wote tumepotea kama kondoo wasio na mchungaji, unadhani vipi kama kuna ambaye angestahili kupokea baraka yoyote kutoka kwa Mungu au kupata uzima wa milele kwa hali hii tuliyonayo.

Na jambo la kujua ni kwamba hatujaanza kupotea baada ya kuzaliwa, hapana! tulishapoteaga siku nyingi sana baada tu ya Adamu kuruhusu dhambi ndani yake…huko ndiko tulipotea kwasababu tulikuwa katika viuno vyake.. hivyo tunakuja kuzaliwa tu na dhambi zetu.

Warumi 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”;

Unaona!, Ndio maana Mungu alipochungulia toka juu aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu, hakuna hata mmoja! Kwasababu wote tumepotoka, tumeoza wote pamoja, Hakuna hata mmoja mwenye haki. Kilichokuwa kimebakia ni sisi tu kwenda kutupwa kwenye ziwa la moto habari yetu ishie hapo.

Lakini BWANA YESU kwa upendo wake mkuu ilimgharimu aje hapa duniani atununue kwa gharama zake na kutufanya washirika wa urithi wa baraka za Mungu (akatu-adopt).

Ulishawahi kuona mtu ambaye ni tajiri sana hana watoto, anakwenda nchi ya mbali kutafuta mayatima ambao maisha yao yapo hatarini na kuwaleta kwake na kuwafanya kuwa wanawe? (anawaa-adopt)..Ndio hicho hicho, Bwana Yesu alichokifanya kwetu…alitutwaa sisi ambao tayari tulikuwa tumeshatamkiwa hukumu na kutufanya kuwa wake.

Hivyo ilimpasa aje kama mwana-kondoo asiye na hatia yoyote, asiye na dhambi yoyote..aje achijwe kama sadaka ya kutusafisha/kutuondolea dhambi. Kama ilivyo kanuni ya kiroho pasipo kumwagika damu hakuna ondoleo la dhambi (Soma Waebrania 9:11-28)

Na kama vile kondoo wanaponyolewa manyoya yao kwa ajili ya sufu au wanapopelekwa machinjoni wanakaa kimya tofauti na mbuzi, ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu, alitukanwa hakurudisha, alipigwa makofi hakurudisha, alitemewa mate, hakurudisha, japo alisikia maumivu kama mwanadamu mwingine yeyote lakini aliishia na kusema BABA WASAMEHE. Hii ilitoka ndani ya moyo wake kabisa na sio kinafiki.

Nabii Isaya alimwona miaka mingi sana kabla ya kuja kwake akaeleza habari zake..

Isaya 53:3-8 “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; MTU WA HUZUNI NYINGI, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

4 HAKIKA AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU, AMEJITWIKA HUZUNI ZETU; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.

7 Alionewa, lakini ALINYENYEKEA, Wala hakufunua kinywa chake; Kama MWANA-KONDOO APELEKWAYE MACHINJONI, Na kama vile kondoo ANYAMAZAVYO Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, HAKUFUNUA KINYWA CHAKE.

8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu;”

Na ndio hapa sasa Yohana Mbatizaji anamshudia akisema…

“…Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”

Na Yohana mtume pia alimuona katika maono kama mwana-kondoo aliyechinjwa kwa ajili yetu sisi tuliokuwa tumepotea.

Ufunuo 5:6 “Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, MWANA-KONDOO AMESIMAMA, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

[7]Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.

[8]Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.

[9]Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ULICHINJWA, UKAMNUNULIA MUNGU KWA DAMU YAKO WATU WA KILA KABILA NA LUGHA NA JAMAA NA TAIFA,

[10]ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

[11]Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,

[12]wakisema kwa sauti kuu, ASTAHILI MWANA-KONDOO ALIYECHINJWA, KUUPOKEA UWEZA NA UTAJIRI NA HEKIMA NA NGUVU NA HESHIMA NA UTUKUFU NA BARAKA.

[13]Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.

[14]Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.” (Haleluya)

Unajua kwa undani ni kwanini maandiko yanasema, Bwana Yesu alipigwa kwaajili yetu?

Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”

Sio kwamba Mungu alikuwa anataka kutuhukumu ndio akaona amtafute mwanae aje kufa kwa ajili yetu Hapana! Ni kwamba tayari Mungu alikuwa ameshatuhukumu, adhabu ilikuwa imeshapitishwa.. ilikuwa ipo njiani kutufikia, na ndipo Bwana Yesu akaingilia kati kufa kwaajili yetu.

Ni sawa na mtu ambaye tayari amesharusha jiwe kumlenga mwingine, na lile jiwe wakati lipo njiani kumfikia mlengwa, anatokea mwingine kukubali kupigwa kwa niaba ya Yule aliyekusudiwa kupigwa jiwe hilo. Ndicho Bwana Yesu alichokuja kukifanya.. Hakuja kuifuta hukumu, bali alikuja kuichukua ile hukumu na kuwa yake.. ndio maana ilikuwa hana budi afe!.. achijwe kama kondoo.

Hivyo kile kifo hakikuwa cha kwake, hakukusudiwa yeye, kilikuwa ni chetu tulikusudiwa sisi, ile aibu haikuwa ya kwake ilikuwa ni yetu!… Yale maumivu hakukusudiwa yeye, tulikusudiwa sisi, kifo cha mateso hakukusudiwa yeye, tulikusudiwa sisi.. Maana yake ni kwamba endapo, Mwokozi Yesu asingetokea.. ni kipindi kifupi sana mbele yetu kilikuwa kimebaki.. ghadhabu ya Mungu ingetumaliza wote, tungekufa kikatili na kwa aibu kama watu wa gharika, na sodoma na ghomora, tungesikitika, na kulia, na kuhuzunika, na kuteseka kwa maumivu, na hatimaye kufa na kuishia katika lile ziwa la moto.

Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote”.

Kumbuka hapo maandiko yanaposema “Ameyachukua masikitiko yetu”.. haimaanishi magonjwa yetu, wala shida zetu, wala huzuni tulizo nazo sasa, wala masikitiko tuliyonayo… La! Haimaanishi hivyo, (ingawa si kosa kutafsiri hivyo), lakini maana yake ya awali kabisa sio hiyo bali inamaanisha zile huzuni ambazo tungezipata baada ya sisi kupigwa na Bwana, na yale masikitiko ambayo tungeyapata baada ya kuipata ile adhabu ya Mungu.. yeye ndiyo kayachukua hayo.. yeye ndio atahuzunika badala yetu baada ya kupigwa na Mungu, yeye ndiye atasikitika katika kuadhibiwa kule.. hiyo ndio maana ya kubeba masikitiko yetu..

Ndio maana kuna mahali Bwana Yesu alisema “nina huzuni nyingi kiasi cha kufa, Marko 14:34”

Umeona umuhimu wa Yesu kwetu?… Je unamthamini Bwana?..bado tu hujaona umuhimu wa Yesu maishani mwako?

Kumbuka ghadhabu ya Mungu bado ipo, tena ina nguvu mara dufu kwa wale wote wanaoidharau kazi ya msalaba..

Waebrania 10:29 “Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”

Umempokea Yesu?.. Kama bado unasubiri nini?.. kumbuka mlango wa neema hautakuwa wazi milele.. ingia leo ndani ya safina, kwa kutubu dhambi zako zote, ukimaanisha kuziacha na ubatizwe ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo, na upokee kipawa cha Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

  1. Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *