Tena ufalme wa mbinguni umefanana na..!
Shalom, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tujifunze maneno ya uzima.
Sehemu ya 01.
Katika kitabu cha Mathayo sura ya 13 Bwana Yesu alizungumza mifano saba 7 kuhusu siri za ufalme wa mbinguni umefanana na…. Lengo kuu Yesu Kristo alitaka tutafakari kwa kina hiyo mifano ili tupate siri ziliyomo ndani.
Sasa katika sehemu hii ya kwanza tutachambua kwa undani mfano mmoja na tutaendelea na mingine..
Siri ya 01.
Mathayo 13:44
“Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
”
Hapa Bwana Yesu anasema ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika, kumbe lazima tufahamu ufalme wa Mbinguni ni hazina na sio hazina pekee lakini ufalme wa Mbinguni umesitirika(sio kwamba umefichwa mahali watu wasiuone ila mtu atakaekusudia kuutafuta ataupata)
Lakini anaendelea kusema kwamba kuna mtu(mfanya biashara aliiona hiyo hazina) umewahi kufikiria kwa nini baada ya huyo mtu kuiona katika shamba asiende kuichukua? Lakini ilimbidi akauze kila kitu alichonacho ili alipate lile shamba ili apate ile hazina iliyoko ndani ya shamba lile..
Maana yake nini? Ufalme wa mbinguni upo na unaweza ukauona lakini ukashindwa kuupata japokua uliuona/umeuona maana yake kuna kanuni ya kuweza kuupata pasipo kufata kanuni hutaweza kuupata haijalishi umeuona. Kuna hatua za kufanya ili uupate..
Sawa sawa na mtu aliienda mgodini kuuona mgodi haimaanishi tayari ameipata dhahabu ili aipate inahitaji aingie gharama..
Na ili uupate unahitaji kuuza kila kitu maana yake kuna gharama za mtu kuupata ufalme wa mbinguni. Tutaona tunatakiwa kuuza kila kitu kipi?!
Sasa turudi hapo tujifunze jambo moja kabla ya kuendelea.. juu ya huyu mfanyabiashara. Tuangalie katika pande zote mbili.
1.Mfanya biashara wa kwanza ni Yesu Kristo.
Yesu Kristo ndio mfanyabiashara ambae ilimlazimu auze kila kitu kwa ajili ya kuipata hazina ya thamani iliyositirika shambani(katika ulimwengu huu) ambayo ni mimi na wewe. Ikamlazimu kuacha kila kitu kwa ajili ya kutupata sisi. Na aliuza kila kitu kwa furaha yake baada ya kutambua uthamani na uzuri wa hio hazina alioiona katika shamba (shamba ni ulimwengu huu na hazina ni mimi na wewe)
Ili atupate sisi ilimlazimu kulinunua shamba(kuja ulimwenguni)
Nataka tuangalie kwenye huo huo mstari hapo juu anasema huyo mfanya biashara aliiona hiyo hazina, lakini hakuichukua very strange rudia kusoma hapo anasema akaificha tena maana yake aliiona hakuichukua akaificha vizuri.
kwa furaha yake maana yake hakulazimishwa akaenda akauza vyote alivyonavyo ili alinunue hilo Shamba ili aipate hiyo hazina yote.
Tunaona Yesu Kristo alikubali kuacha kila kitu(yaani Mungu anakubali kutoka kwenye kiti cha enzi, anakuja duniani, anakuwa hana utukufu anapigwa,anadharauliwa tena na viumbe alivyoviumba mwenyewe anasurubiwa nk)
1 Timotheo 3:16
Tafakari ni upendo wa namna gani Yesu anatuonyesha huu, mawazo ya kusema Mungu yuko mbali na wewe au anakuchukia yanatoka wapi kama sio shetani anachezea akili zako?.
02.Mfanyabiashara wa pili ni mimi na wewe.
Sisi pia ili tusiishie kuuona tu ufalme wa Mbinguni na tukashindwa kuupata kama vile alivyofanya Yesu Kristo (Wafilipi 2:5-10) yeye aliona kuwa ni sawa na Mungu sio kitu cha kushikamana nacho sisi vivyo hivyo tunahitaji kuuza kila kitu kwa ajili ya Kristo.
Tunatamani kuupata ufalme wa mbinguni (kuuteka) lazima tuingie gharama na hapa ndio Wakristo wengi sana bado tunachangamoto lakini kwa uweza wake Bwana sote tutashinda.
Mtume Paulo anasema anahesabu Mambo yote ni hasara kwa ajili ya Kristo(ukiona(ku experience)uzuri, uweza, utukufu,heshima nk ambavyo vipo ndani ya Kristo ukaelewa hapa utakubali kuingia gharama lakini kama hujaona hutaweza kuingia gharama kabisa ndugu yangu tafuta kuona yaliyomo ndani ya Yesu Kristo itakusukuma kuuza kila kitu)
Mathayo 19:21
“Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa *mkamilifu* , enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.”
Neno Mkamilifu hapa anazungumzia Ukomavu maana yake mtu ambae ni matured anaweza kuingia gharama tofauti na mtoto mdogo ambae haelewi thamani ya kitu fulani hawezi ingia Gharama kukipata..
Watu wengi huwa tunamuona huyu kijana kama mjinga lakini sivyo ni kwa sababu alikua hajafahamu vizuri(Mtoto) na Yesu anamwambia ukitaka kuwa Mkamilifu japokua alikua anazishika amri lakini hakua mkamilifu bado na mkamilifu hapa anaezungumziwa ni mtu ambae amekomaa kiroho(sio kukaa katika imani kwa muda mrefu au kukaa katika dini muda mrefu bali mtu anaemuelewa Mungu kwa namna ya Undani sana.)
Mtume Paulo anasema..
Wafilipi 3:7
“Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.”
Alikubali kuuza kila kitu ambacho hapo awali si alikuwa anavipenda kwake na vilionekana kuwa na maana lakini baada ya kuona/experience kuhusu Yesu Kristo anaendelea kusema…
Wafilipi 3:8
“Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;”
Mtu kama huyu alikua ameuza vitu vyake vyote(ndio kaana anasema kuishi ni Kristo kufa ni faida) ili kupata hazina ya thamani iliyositirika ambayo ni Yesu Kristo mwenyewe. Maandiko yanasema hazina zote zimesitirika ndani yake.
Je! Na sisi tuko tayari kukubali kuuza kila kitu(Kristo akisama acha hiki utaacha?, Maisha fulani uliyoyazoelea utaacha? Nk)kwa ajili ya hii lulu ya thamani kuu ambayo ni Yesu Kristo?
Katika sehemu ya pili tutaendelea kuangalia mfano mwingine tena.
Omba maombi haya kwa uchache na kwa imani kabisa.
“ Bwana Yesu ninaomba unisaidie,unifungue macho yangu nipate kuona uzuri/ku experience uzuri ulio ndani yako, niongezee neema ndani yangu ya kukubali kuingia gharama ya kuuza vitu vyangu vyote kwa ajili yako, ninakushukuru Bwana Yesu, maana unanipenda,unanijali na kunidhamini ninaamini nguvu hiyo nimepokea ndani yangu ni katika Jina la Yesu Kristo Bwana wangu amen”*
Tumia muda mwingine kuomba mwambie Bwana Yesu yale uliyojifunza na kuelewa na angalia mambo gani yanayosababisha ushindwe kulipa gharama/kupiga hatua katika wokovu wako Bwana akusaidie.
Tukutane katika sehemu ya pili.
Bwana Yesu akubariki sana
Maranatha.
@Nuru ya upendo,
Mawasiliano:0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.