TUNAJIFUNZA NINI KWA MKE WA LUTU?

Biblia kwa kina No Comments

Shalom, nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.

 

Katika biblia kila habari tunayoisoma inafundhisho kubwa sana nyuma yake ambalo Yesu Kristo anatamani sana tulifahamu na tujifunze kupitia hao ili na sisi tusije tukarudia makosa yale yale yaliyofanywa na wao hapo mwanzo.

 

Hivyo kila habari unayoisoma katika maandiko usiichulie kama stori Fulani tu basi ukaiacha bali itafakari kwa kina kuna kitu Roho Mtakatifu atakufundisha.

 

Katika habari hii tunaona malaika wanaingia sodoma kwenda kuiangaimiza kutokana na maovu ya watu waliokuwa wakikaa ndani yake. Yalifikia katika kiwango cha juu sana. lakini alipatikana mtu mmoja Lutu ambae alikuwa na hofu ya Mungu na ni mcha Mungu(alionekana mwenye haki mbele za Bwana) lakini pia Mungu alimpa nafasi Lutu ya kuwahubiria hata wakweze

 

Mwanzo 19:14” Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze.”

 

Unaona hapo Lutu aliwahubiria wakweze lakini hawakumuelewa(walimuelewa lakini walipuuzia kama watu wa ulimwengu huu wa sasa wanavyopuuzia wanavyosikia injili ya Yesu sio kwamba hawaelewi lakini wanapuuza wanaona wanaowaubiria kama wanapoteza Muda na hawana kazi ya kufanya.) wakaona ni kama anaongea kitu kisichokuwa na maana yoyote kutokana na dhambi ilivyokuwa imekithiri na hata ikaziba masikio yaon afahami zao rohoni.

 

Na baadae tunaona malaika wale wanamhimiza sana Lutu afanye hima kutoka katika mji huo na walipoona anakawia kawia walimshika mkono na kumkokota kumtoa katika ule mji. Na waliwatoa yeye pamoja na binti zake na kuwaambia wasigeuke nyuma wajiponye nafsi zao.

 

SASA NI KWA NINI MKE WA LUTU ALIGEUKA KUWA JIWE LA CHUMVI?

Natamani tutafakari kwa pamoja katika sehemu hii.

je umewahi kufikiri sababu ya mke wa Lutu alipogeuka nyuma alikuwa jiwe la chumvi?” je sababu pekee kubwa ilikuwa ni hiyo tu peke yake? Ama kulikuwa na jambo lingine? Maana kugeuka nyuma tu kuna madhara gani? Maana hapo kosa hilo halikustahili Mungu kumpatia adhabu kubwa na kali kama ile.

 

kama maandiko yanavyosema ….

 

mwanzo 19:26 “Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi”

 

Maana haitofautianani sana na uongo walioufanya wakina Ibrahimu, Rebeka kwa kumwambia Yakobo ajifanye kuwa kama Esau ili achukue Baraka za mzaliwa wa kwanza. Lakini tunaona anageuka nyuma na kuwa jiwe la chumvi.

 

Wengi wetu hapa huwa tunafikiri tu kuwa malaika wale waliwaambia wasigeuke nyuma basi wala hakukuwa na kingine ni maneno yale yale walikuwa anasema lakini sivyo.

 

Hapa hawa watu kuna maneno mengine mengi sana(ya kuwaasa na kuwasihi) malaika wale waliwaambia ni kama walikuwa wanawahubiria injili kutoka ndani ya mji mpaka nje ya mji kuna mazungumzo mengi sana walikuwa wakiwaambia lakini biblia haijajayaweka wazi. Kiasi kwamba walielewa vizuri walipewa madhara ya wao kugeuka nyuma itakuwa ni nini(yaani kukaidi maagizo ya Mungu). Siku zote Mungu hasemi kitu na asikielezee na madhara yake kwa undani ili yule anaefikishiwa ujumbe aelewe vyema.

 

Na ndio maana tunaona mwishoni kabisa pale wanawaachia baada ya kuwafikisha nje ya Mji wanasema maneno haya kwako kuwasisitiza tena..

 

Mwanzo 19:17 “ Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, JIPONYE NAFSI YAKO USITAZAME NYUMA, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.”

 

Unaona hapo? Hivyo baada ya kuwaambia maneno yote ama ujumbe wote ndio wanawaambia hivyo.

 

Huenda waliwaambia “ili nafsi zenu zipate kuwa salama msipatikane na madhara yoyote mfike salama basi msigeuke nyuma maana msipofanya hivyo mtaangamia” na ndio maana hap anasema “JIPONYE NAFSI YAKO USITAZAME NYUMA”  kama vile Mungu alivyotangulia kumpa maelekezo Adamu pale edeni kuwa siku atakayokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya atakufa. Na akawa anashuka kusema nae (kumfundisha kila siku jioni).

 

Hivyo mke wa Lutu alikosa utii na kutokuyakubali maneno ya Mungu kupitia malaika wale ingali alitoka sodoma lakini hakuwa tayari kumsikiliza Mungu. au kuti kile alichoambiwa.

 

HII INAFUNUA NINI KATIKA NYAKATI HIZI TULIZOPO?

 

Kwa neema yake Mungu tumeokolewa sote toka dhambini katika utumwa wa shetani na kuwekwa huru katika Kristo Yesu. kama mke wake Lutu alivyookolewa toka sodoma katika uharibifu ule.

 

Hatuna budi kusonga mbele na kuyaamini maneno yote ya mwokozi wetu Yesu Kristo. Tusianze kuangalia nyuma kuanza kuyatamani tena mambo ya kale tuliyoyaacha huko(mke wa Lutu bado alikuwa akitamani mambo ya sodoma moyoni mwake)  tusonge mbele kama tukiangalia nyuma(yaani kuanza kuyarudia yale mambo ambayo tumepewa neema ya kuyashinda, tutageuka nguzo za chumvi rohoni) kumbuka mandiko yanasema mambo hayo yote yalifanyika kwa jinsi ya mifamo ili kutuona sisi hivyo uharisia zaidi uko kwetu.

 

1 wakorintho 10:11” Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zaman”

 

Maandiko yanazidi kutuonya hivyo usiuangalie ulimwengu jiponye nafsi yako ulimwengu huu uko karibu kuanganizwa angalia usije ukatoka sodoma na ukashindwa kufika soari.

 

2 Petro 20:22” Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

[21 ] Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.

[22]  Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”

 

Unaona hapo kwenye mstari wa 21 anasema “Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa

kama mke wa Lutu aliijua amri yote na maelekezo waliyopewa lakini aliyakanyaga akayaona kuwa si kitu kabisa yakamkuta na sisi tuwe makini sana na zaidi sana Neema ya Kristo izidi kuongezeka tuzidi kusonga mbele.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *