Usiache kupaza sauti yako kama tarumbeta.

Uncategorized No Comments

Usiache kupaza sauti yako kama tarumbeta.

Kuna watu wanasema kuhubiri injili masokoni na vijiweni ni kukosa kazi ya kufanya na kwamba watu wanaofanya hivyo hawapo sawa kiakili au ni wavivu wa kufanya kazi.

Lakini wewe ambaye umeitwa kufanya kazi hii ya Mungu, nataka nikutie moyo kwa Neno la Mungu ya kuwa usiache kupaza sauti yako kuwajulisha matendo yao ya giza, haijalishi wanasema nini juu yako we usiwaangalie. Endelea kupaza sauti kama tarumbeta kuwaambia kosa lao maana wao wanaasi sana. Kumbuka taabu yako si bure ijapokuwa utakataliwa sasa lakini Bwana yupo pamoja na wewe kukusaidia na kukulinda.

Isaya 58:1 “Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao”.

Yona 3:4 “Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.

[5]Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo”.

Mitume wa Bwana Yesu walihubiri injili mpaka masokoni kila siku.

“Basi katika sinagogi akahojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu, na wale waliokutana naye sokoni kila siku.” (Matendo 17:17)

Bwana wetu Yesu Mwenyewe alitembea mtaa kwa mtaa kuhubiri injili.

“Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu…” (Luka 8:1)

Kikawaida ni ngumu kumsimamisha mtu barabarani na kumwambia asikilize. Lakini unapohubiri bila hata ridhaa yake, Neno linaweza kuingia ndani yake hata kama hataki. Lile Neno linaweza kuwa mbegu njema itakayochipuka kwa wakati wake.

Kwahiyo ni heri asikie moja kuliko kutokusikia kabisa.

Wapo watu ambao wanapaswa kusikia injili kwa lazima hata kama hawataki kusikia.

Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana” (Ezekieli 2:7)

Kazi ya kuhubiri si nyepesi. Lakini matokeo yake ni makubwa sana:

“Kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye” (Luka 15:10)

Bwana akubariki askari wa Bwana. Kazi yako ni njema sana.

“… Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! (Warumi 10:15).

Amani ya Kristo ikae nawe (Maranatha.)

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *