USIFANANE NA TOMASO.

Biblia kwa kina No Comments

Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Liko jambo kubwa sana kujifunza kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu Kristo.

Tomaso hakuwa na tabia ya wizi,au usaliti Kama ilivyokuwa kwa Yuda Iskariote lakini iko tabia ambayo alikuwa nayo tofauti kidogo na wenzake.

Lakini pia Tomaso alikuwa lazi hata kufa pamoja na Bwana Yesu pale aliposikia taarifa hizo. Maana yake alikuwa na upendo wa dhati kabisa na Bwana wetu Yesu Kristo.

Yohana 11:16“Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye.

Unaona hapo? Aliwahimiza hata wenzake nao wakafe pamoja na Kristo msalabani. Hapa Tomaso hakuwa anasema kwa unafiki bali alikuwa anamaanisha kabisa.

Lakini tabia pekee aliyokuwa nayo na ilimgharimu kwa sehemu kubwa ni kutokuamini uweza wa Mungu yaani Alikuwa na mashaka na uweza wa Mungu.

Na jambo hili lilipelekea yeye mwenyewe kupoa katika shughuli mbali mbali za kiutumishi kama mtume alieteuliwa na Bwana Yesu. 

Hakuwa anaamini kabisa kama Yesu atafufuka na hata hata alipoambiwa kuwa Yesu amefufuka hakutaka kuamini kabisa juu ya jambo hilo.

Hivyo alipoitwa na wenzake mitume wakusanyike waombe wala hakuwa na muda huo kutokana na mashaka yaliyokuwa yamejenga ndani yake imani kuwa Bwana Yesu hawezi kufufuka..

Hata wenzake walipokuwa wakitafakari Habari za Yesu Kristo yeye alikuwa hayupo amejitenga kivyake vyake kifupi hakuwa anataka kabisa ushirika tena na wenzake.

Na mwisho wa siku Yesu anawatokea wanafunzi walipokuwa katika sehemu ya kiibada Tomaso yeye hakuwepo na hata walipomwambia yote yaliyotokea hakuwamini kwa sababu moyo wake ulikuwa tayari umeshapoteza tumaini kabisa.

Yohana 20:24  Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu.

25  Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.

26  Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu

27  Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.

Ni nini Tunajifunza kutoka kwa Tomaso kama watu tuliomwamini Yesu Kristo?

Tusiwe ni watu wa kujitenga kwa kutokuhudhuria makusanyiko. Hata kama unaona hakuna tumaini lolote umechoka na kuumizwa na kukata tamaa usiache kukusanyika kama maandiko yanavyosema Waebrania 10:25.

Epuka udhuru maana ni hasara kwako wala sio kwa mchungaji wala shemasi au Mungu ni hasara.

Kumbuka unapodumu na wenzako katika maombi,ibada nk iko nguvu na Neema ambayo kama mwili wa Kristo mnapokuwa pamoja Kristo anaiachilia.

Kumbuka unapokuwa mtu wa kujitenga unakaribisha uwepo wa shetani karibu yako. 

Maana ni sawa na kondoo aliejitenga na kundi ni lazima tu atakutana na wanyama wakali(ibilisi) watamlarua vibaya sana. 

Shetani atakuhubiria jitenge na kundi na utakuwa sawa tu utafanya ibada na utakuwa sawa sio lazima ukusanyike. Ndugu tambua shetani anakuweka mawindoni mwisho atakunasa kama usipoamua kubadilika.

Tomaso alilifahamu na ndio maana tuona katika siku hiyo akakubali kuwa na wenzake na Bwana Yesu akatokea na akafunguliwa macho na kumfahamu vyema Yesu Kuwa yeye ndie Elohimu mwenyewe. 

Hivyo ndugu dumu na wenzako katika hali zote utamuona Mungu katika nyakati zote na atakutia nguvu. Kujitenga mwenyewe kwa sababu mchungaji au mpendwa mwenzako sio suruhisho bali maangamizi..

Maranatha. 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *