USIYAKUMBUKE MAMBO YA ZAMANI

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Kama watu tuliozaliwa mara ya pili ni wazi kuwa kuna mambo mengi tumewahi kuyafanya au kufanyiwa kabla hatujampokea Yesu Kristo.

Mengine huenda yaliyawahi kutokea tukiwa katika wokovu kwa kuanguka katika dhambi fulani na nk.

Sasa maandiko yanatusisitiza kama wana wa Mungu tusiyakumbuke wala kuyatafakari mambo ya zamani(yaliyokwisha kupita).. Sasa ni kwa namna gani tusiyakumbuke? Je tuyafute katika akili zetu iwe kama hayakuwahi kutokea? Jibu ni la!

Maana hatuwezi kusema tunasahau kila kitu na kweli vikafutika hapana ubongo unahifadhi kumbukumbu na si rahisi kufuta. Sasa maandiko yanasema…

Isaya 43:18“Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.”

Sasa kwa nini biblia inasema tusiyakumbuke? Ni nini maana yake na ni kwa namna gani tunaweza tusiyakumbuke?

Maana yake ni kwamba tusiweke umakini na kuanza kufikiria/kuyafikilia mambo ya zamani  tuliyowahi kufanya au kufanyiwa..

Hivyo tusiweke umakini sana katika kutatafakari maana unapoweka umakini na nguvu kubwa katika kulitafakari ni wazi kwamba kuna mambo mengine mengi yanazaliwa ambayo yatazidi kuleta shida katika maisha yako.

Lakini maana nyingine zaidi na ambayo ipo katika Mstari huu ni kwamba inapozungumziwa tusiyakumbuke/kuyatafakari mambo ya zamani maana yake ni “kutaka kuyafanya mambo ambayo tayari umeshayaacha

Hivyo pale unapotaka kuyafanya mambo ya zamani ni wazi kuwa unayakumbuka/kujikumbushia na huwezi kutaka kuyafanya mambo hayo pasipo kuanza kuyatafakari kwanza. “Hivyo unapotafakari sana ndio msukumo wa kutaka kufanya unavyozidi kuongezeka sana. “

Hivyo usitoe nafasi katika akili yako kuanza kufikiria sana mambo ambayo ulishayaacha.. kama vile uzinzi, ulevi, uasherati, kufatilia mambo ya kidunia nk. Ikiwa tayari umeshayaacha jitahidi sana kuyaepuka mawazo hayo yanapokuja kwa wewe kutoruhusu sehemu kubwa ya fahamu zako kuzama huko.

Fahamu zako zinapozama huko unampatia nafasi ibilisi ya kukuchochea ujikute unarudi kuyatenda yale mambo ambayo tayari umeshayashinda. Shetani siku zote anatumia milango ikiyo wazi kukushambulia wewe uliyemwamini Yesu Kristo ili akuangushe.

Hivyo kuwa makini sana fikra zako zinapohama na kuanza kukumbuka raha za uasherati,uzinzi,Kamari,wizi nk jitahidi sana kuyashinda mawazo hayo hasa kwa kuomba na kusoma na kutafakari neno utajikuta unamfukuza shetani na anatoka kabisa.

2 Wakorintho 5:17“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”

Hivyo ikiwa sisi tulio katika Kristo Yesu tumekuwa viumbe vipya maana yake hapo kwanza tulikuwa viumbe vya zamani ambavyo vilikuwa vinaenenda gizani na Sasa tumekuwa ni viumbe vipya hatuna budi kuenenda nuruni kwa kujitenga na maovu kila siku tuzidi kupiga hatua mbele zaidi..

Hivyo tusiruhusu Fahamu zetu kutawaliwa na mambo maovu yasiyo faa. Kumbuka kadili unavyopata nafasi ya kuyakumbuka mambo ya zamani (maovu uliyokuwa ukiyafanya ) ndio unavyozidi kubadilika pole pole na mwisho wa siku utajikuta unayarudia.

Iko nguvu kubwa sana katika kutafakari na inaleta matokeo makubwa sana katika roho na katika mwili pia.

Vivyo vivyo kadili unavyozidi kutafakari zaidi mambo ya rohoni ndio unavyozidi kubadilishwa na kufanywa upya ndani yako. Na unazidi kuwa mtu mwingine unayetembea katika mapenzi ya Mungu.

Unapotafakari hata makosa ambayo uliyatenda kabla ya kuokoka na baada ya kuokoka yanakuwa yanakutesa wewe na unampa shetani nguvu ya kukukandamiza lakini Mungu yeye ameshakusamehe tayari muda mrefu sana tangu ulipoamua kugeuka na kuacha njia hiyo uliyokuwa unaipitia.

Fikra zako na fahamu zako zitaendelea kukutesa kama usipokuwa ni mtu wa kusonga mbele na kumtumaini Mungu katika nyakati zote.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *