YAHESABU KUWA HASARA KWA AJILI YA KRISTO.

Biblia kwa kina 1 Comment

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

 

Kuna mambo mengi kabla hujampa Yesu Kristo maisha yako yalikuwa ni ya muhimu naya msingi sana. Kiasi kwamba uliona ni sehemu ya maisha yako. ulijua wakati mwingine ukaaminishwa/nakuamini kuwa hayo ndio yanayoweza kukusaidia.

 

Mambo ambayo haikuwa rahisi kuyaacha na ulikuwa unayaona kama faida katika misha yako kuwa ni ya muhimu sana. Lakini kwa kuwa umemuamini Yesu Kristo basi huna budi mambo yote hayo kuyaona kama hasara kwako kwa ajiri ya Kristo wala usije shikamana nayo maana yatakuweka mbali na Kristo.

 

Kuna mambo ni lazima kama mtoto wa Mungu ukubali kuyaachilia maana hayana msaada wowote kwako na zaidi sana yanakuchukulia muda Mwingi na kukufanya kuwa mchanga kiroho na kuwa mtu wa kutokupiga hatua yoyote ile katika roho.

Mambo ambayo uliweka matumaini katika hayo na kuona ndio kila kitu kwako kama ukiendelea kushikamana nayo na kuyawekea tumaini basi uko katika hatari kubwa sana ya kuabudu sanamu.

 

Mambo ambayo unatakiwa kuyahesabu na kuyaona kama hasara (yaani usiweke tena matuaini katika hayo).

 

  1. Elimu.

Ikiwa elimu ndio ilikuwa inakufanya uone kuwa ndio kila “ufunguo wa maisha” basi sasa ufunguo wa maisha kwako ni Yesu Kristo isiitumainie elimu uliyonayo “sio kwamba haihitajiki la! Ni nzuri sana kuwa nayo na ni vyema kila mtu akawa nayo”. Lakini matumaini yako yasiegemee huko kabisa.

 

Elimu na maarifa yote ya ulimwengu huu ikiwemo sayansi(technologia),philosophy,theologia nk zote mbele za Mungu ni upumbavu maana haziwezi kukupa uzima wa milele.

1 wakorintho 3:19 “Maana HEKIMA YA DUNIA HII NI UPUZI MBELE ZA MUNGU. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.”

2. Fedha.

Vivyo hivyo ikiwa ni pesa ndio ulikuwa unaona ndio kila kitu ukiwa nayo unaweza fanya chochote na hakuna kinachoshindikana. ndugu badili fikra zako sasa muoneYesu kuwa ndio kila kitu katika maisha yako na kwamba ukiwa naye hakuna chochote kile kinachoshindikana HALELUYA..  usije ukaweka matumaini yako kwenye fedha weka matumaini yako kwa mwokozi peke yake maana yeye ndio mambo yote ndani ya yote na katika yote.

 

Daudi anasema..

Zaburi 20:7 “Hawa wanataja magari na hawa farasi, BALI SISI TUTALITAJA JINA LA BWANA, MUNGU wetu.”

Katika jina hili ndipo kuna kila kitu hivyo kama mtoto wa Mungu usiiweke mbele fedha ukawa ni mtu wa kuipenda fedha kuliko Mungu itakughalimu pakubwa sana. Hesabau kuwa unaweza kila kitu katika yeye kama Paulo anavyosema (Wafilipi 4:12).

 

Sio kwamba fedha ni mbaya ama si vizuri kwa mtoto wa Mungu kuwa na Fedha au kuwa tajiri. Lakini matumaini yako na akili yako visijae fedha bali vijae Kristo tu hayo mengine atakuzidishia.”

3.kazi

Pia katika kazi, ikiwa uliona kazi kwako ndio kila kitu pasipo hiyo kazi huwezi ukaishi. Ndugu sema kuanzia leo hata pasipo kazi unaweza kuishi maana chanzo  cha uhai wako sio kazi wala kitu kingine bali ni Yesu KRISTO, haleluya…

 

Ikiwa wana wa Israeli waliishi jangwani miaka 40 lakini hawakufa njaa wala hawakutembea uchi kwamba hawana mavazi wakala milo mitatu kwa kadili ya walivyotaka wao vipi kuhusiana na wewe? je Mungu hawezi kuyafnya hivyo kwako(Yeremia 32:27). Kazi yako kwa sasa ni Kristo fanya kazi yake.

 

sio kwamba ni vibaya kuwa na kazi la! Bali unapoweka tumaini na kuona kazi ndio kila kitu ni makosa makubwa unafanya.”

 

Leo hii watu wakifukuzwa kazi wanaumia sana na kulia zaidi ya wanavyomtenda Bwana dhambi. Hawasikitiki sana na kulia sana pale wanapokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

 

Kwa kusema hivi simaanishi usifanye kazi. Kazi fanya tena kwa uaminifu wote ila usiweke tumaini huko na kuona pasipo kazi huwezi, hesababu kuwa ni hasara  maana unae Kristo.

 

ANASA NA MAMBO YA KIDUNIA YAHESABU HASARA.

 

Anasa za kidunia kama vile fashion na mitindo ya kidunia kama unyoaji ya viduku,kuvaa nusu uchi,mawigi,lipstick,miziki ya kidunia,matusi,uongo,uzinzi,usengeng’enyaji, vyote hivi hesabu kuwa ni hasara na viache kabisa maana havina faida tena kwako zaidi sana ukiendelea navyo ni hasara kubwa maana ukiendelea kushikamana navyo vinafanya Kristo atukanwe katika mataifa na nuru yako inaangaza nini kwa mataifa wasiomjua Kristo,

 

Tamthilia za kidunia,mipira, hivi vitu vyote ndugu kubali kuvihesabu kama hasara maana havina faida kwenye maisha yako tena. Vinakupotezea muda zaidi sana havikujengi vinakubomoa kabisa maana unaweza kukesha navy usiku kucha lakini huwezi kukwesha maobi usiku kucha ukiwa magotini pa Mungu.

 

Musa alihesabu mambo yote ni hasara kwa ajiri ya Kristo Yesu. akaacha utajiri wote na mambo yotye na mifumo na elimu yote ya misri akamchagua Kristo.

 

Vivyo hivyo Paulo aliona mambo yote kuwa kama Mavi kwa ajiri ya Kristo hivyo ndugu yangu mimi na wewe hatuna budi kuviacha na kuamua kweli kweli kumtumikia Mungu.

 

Wafilipi 3:8” Naam, zaidi ya hayo, NAYAHESABU MAMBO YOTE KUWA HASARA KWA AJILI YA UZURI USIO NA KIASI WA KUMJUA KRISTO YESU, BWANA WANGU; AMBAYE KWA AJILI YAKE NIMEPATA HASARA YA MAMBO YOTE NIKIYAHESABU KUWA KAMA MAVI ILI NIPATE KRISTO;”

 

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

One Reply to “YAHESABU KUWA HASARA KWA AJILI YA KRISTO.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *