hizi ni sifa za mtu aliyesamehewa kweli dhambi zake.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu, ambalo ndilo Uzima wetu,

Wewe kama mwamini, umeokoka kwa kumpokea Bwana Yesu maishani mwako, una kila sababu za kuhakikishia usalama wa wokovu wako, isifike mahali ukaridhika tu kisa umemkiri Yesu kwa kinywa chako, au kwasababu umesamehewa dhambi zako, hapana bali unatakiwa ujae maarifa zaidi ya hapo, kwa kuwa wokovu haupo tu kwa kuamini na kusema Yesu alikufa kwa ajili yangu, hapana,

Ikiwa utaendelea kuamini hivyo,basi fahamu pia na meshetani, yaani mapepo,nayo yanaamini Yesu alikufa kwa ajili ya ulimwengu, tena yanaweza yakawa yanaamini zaidi yako wewe, na hiyo itakuwa ni Imani bure, isiyoweza kufanya chochote, soma Yakobo 2:19, jiulize katika Imani hiyo je na hao wamesamehewa makosa yao, kwasababu wanaamini kifo chaYesu,

Yapo Mafundisho potovu yanayoendelea kuwapotosha wengi, kwamba waamini tu kazi ya Yesu msalabani,au waamini tu msamaha wa dhambi, alafu basi, baada ya hapo waendelee na maisha yao, jambo ambalo si kweli na hizo sio sifa za wewe kusema umeokoka na kumpokea Bwana Yesu..

Tukiliangalia hili neno “Kuamini” kwa kugha ya kigiriki ni PISTIS, yenye maana zaidi ya kusema tu unao ujasiri wa kumkaribia Mungu, lakini hili limeenda mbali zaidi na kukufanya uwe mwaminifu, hiyo itakufanya uwe na ujasiri wa kusema unamwamini Yesu lakini pia una Uaminifu na yule unayemwamini,

Yule aliyemwamini Yesu Kristo yapo mambo utayaona ndani yake,

NI KONDOO

Sote tunaifahamu tabia ya kondoo, sio kama mbuzi, kondoo yupo tayari kuchungwa na anakubali kupelekwa kule anakotaka Mchungaji wake, tofauti na mbuzi, yeye sauti ya kusikiliza hana, anajichunga mwenyewe, na wewe kama umeokoka halafu unatabia ya mbuzi,basi fahamu bado ujaokoka,bado ujaamini,

Yani bado ujapokea msamaha wa dhambi, lazima aisikiize sauti ya Mchungaji wake ikimuelekeza jinsi anavyopaswa kuishi, lazima ajue jinsi ya kukaa mbali na dhambi na mambo yote maovu, mtu kama huyu ni vema aendelee kufundishwa zaidi ili toba ya kweli iumbike ndani yake..

Yohana 10:2 Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.

3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.

4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.

5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni…

27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.

29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

NI KIUMBE KIPYA,

Maandiko yanasema tazama yakale yamepita nasasa yamekuwa mapya,

2 Wakorintho 5:17

[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Umeona hapo, ukiwa ndani ya Kristo unakuwa kiumbe kipya, maana yake unauvua ule utu wote wa kale unauvaa utu upya tena ni ule unaofanana na Kristo kwa kuwa tayari upo ndani yake, haiwezekani ukawa ndani ya Yesu Kristo halafu ukawa na mwenendo tofauti na yeye, lazima utaziiga tabia zake tu,

kama maandiko yanavyosema mtakuwa watakatifu kama Baba yenu, basi lazima na wewe uliyefanyika kiumbe kipya utakuwa na viashiria ndani yako vya kutaka kuishi kama Baba yako alivyo,

Utapenda kuishi kama Baba yako na kutafuta kuishi kama yeye, shauku yako itakuwa ni ufanane na Bwana, kwasababu tayari ndani yako umekuwa mpya, ni jambo lisilowezekana kwa mtu aliyefanyika kuwa kiumbe kipya alafu bado anaishi Maisha ya uduniani,

yani mambo bado yupo na mambo maovu ya hu ulimwengu, pengine haonyeshi dalili zozote za kupiga hatua kwenye wokovu ili afanane na Baba kwenye ukamilifu, sasa huyu kiuhalisia bado ajafanyika kiumbe kipya.

Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.

13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu

1Yohana 3:9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu

ATAKUWA MWANAFUNZI,

Hii ni sifa anayotakiwa nayo huyu mtu aliyempokea Yesu, lazima afahamu Katika hatua za mwanzo kabisa za kuokoka kwake,ni vema akajijua yeye ni mwanafunzi, na kama ni mwanafunzi lazima akae chini kufundishwa, kujifunza ili aweze kukua na kuongezeka kimaarifa ya kumjua Mungu,

Matendo 2:41  Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

42  Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

Unapookoka tambua jukumu la kufatiliwa, jukumu la kuchungwa yaani kuwa chini wa watumishi watakaokulea, kukusaidia au kuyajua maendeleo yako ya rohoni ni lazima, lakini ukiona hupendi shirika na wapendwa wenzako,ndo Kwanza ukiwaona unakimbia au unatoa kisingizio, sio mtu wa ibadani au kupenda kufundishwa, fahamu kabisa bado ujamwamini Yesu Kristo..

Ni wakati wako wa kujitathmini maisha yako je, una sifa za kusema umeokoka,una sifa za kusema nimempokea Bwana Yesu moyoni, ukijiona una sifa hizo basi tambua ni Mungu aliye ndani anakuthibitisha kuwa wewe ni mwana wake, na Yesu Kristo tayari kashafanyika wokovu ndani yako, ni kuendeleza bidii ya kusimama kwenye Imani,

Lakini ukijiona hauna sifa hizo, yaani sio kondoo, siyo kiumbe kipya,sio mwanafunzi, basi unamuhitaji Yesu Kristo haraka sana, kwasababu bado hujaokoka, ni wakati wako sasa, Neema ya Bwana Yesu inakuita upate kutubu kwa kumaanisha , maanisha kabisa ndani ya moyo wako ukihitaji badiliko la kweli na Yesu mtenda miujiza atakuokoa leo,

Ikiwa utatamani kuokoka,au kumpokea Bwana Yesu moyoni mwako,tutafute kwa namba zetu chini ya somo hili,na Mungu akubariki…

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *