′Unawezaje kufahamu mambo ya Rohoni

Biblia kwa kina No Comments

Unawezaje kufahamu mambo ya Rohoni.

nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari katika Makala fupi namna ya kuyafahamu mambo ya Rohoni. Nakuombea neema ya kuelewa katika kila utakachokwenda kujifunza.

Wakristo wengi tunatamani sana kuyajua mambo ya rohoni kujua jinsi ulimwengu wa roho unavyofanya kazi nk. Na wakati mwigine tunafikiri ni kazi sana au haiwezekani au ni ngumu sana kufahamu labda mpaka ujitahidi sana ufunge siku tatu au saba kavu kwa ajili ya kufikia kuyajua mambo ya rohoni lakini ukweli ni kwamba sivyo hivyo kama tunavyofikiri wengi wetu.

lazima kwanza tufahamu sio kazi ngumu kujua mambo ya rohoni, na fahamu ni muhimu sana kuelewa Mungu hajaweka kitu kwetu ili kiwe kigumu kukifikia au kukielwa, ulimwengu wa rohoni upo kwa ajili yetu pia na ndio sehemu ambayo tunatakiwa kuifahamu kwa kina na kuliko hata ulimwengu huu wa mwilini.

na ukweli ni kwamba Mungu hajatuficha kwamba tusijue la! Bali Mungu anatamani sana sisi tufahamu lakini sisi ndio hatujawa tayari.

mtu anaweza kuwa anafunga na kuomba na kila siku lengo akue na kujua hasa kuhusu ulimwengu wa rohoni lakini asifanikiwe kufahamu kwa sababu hajawa tayari.

Ni kwa namna gani mtu afanye mambo yote hayo na na nikwambie hajawa tayari? Ndio mtu anaweza kufanya yote hayo lakini bado asiwe tayari. Kwa namna gani sasa?

Mungu kaweka wazi sana kuhusu mambo ya rohoni yanavyofanyika kwa kutumia mazingira haya haya yanayotuzunguka, kwa kupitia asili ya vitu vilivyo katika ulimwengu huu, miti,wanyama,utawala nk haya mambo yote kama mtu ataweka umakini na kujifunza kupitia haya basi huyo mtu ataweza kupata picha kamili katika ulimwengu wa roho kuna nini na ukifanya hivi na vile utajikuta katika hali gani.

ulimwengu wa kiroho una mifumo kanuni na utaratibu zake kama jinsi ulimwengu huu tunaoishi(natural world) kama vile mtu asipofata sharia na taratibu za ulimwengu huu atajikuta anapata madhara vivyo hivyo hata katika ulimwengu wa rohoni.

na mambo ya rohoni nini? Ni mambo yanayohusu Mtu wa ndani, asili na sehemu ambayo yeye anaishi au mfumo mzima wa uhalisia wa maisha ya mtu wa ndani. Au kwa maana rahisi ni kujua mfumo mzima na uhalisia wa ulimwengu unaomuhusu mtu wa ndani.

Mtu wa ndani anaishi na ku-operate katika ulimwengu wa  roho na mtu wan je naishi na ku-operate katika mazigira haya yanayotuzunguka hivyo mtu wa ndani ana dunia/ulimwengu wake na mtu wa ndani ana dunia/ulimwengu wake.

Unawezaje kufahamu mambo ya rohoni/kujua uhalisia katika ulimwengu wa rohoni na kufanya usiwe mtu wa mwilini?

maana mtu asipojua mambo ya rohoni maana yake hawezi akaishi maisha ya rohoni maana yake atakuwa ni mtu wa mwilini na akiwa mtu wa mwilini atashindwa kufahamu mambo ya rohoni atajikuta kila siku kwenye mitego ya shetani.

1.kuwa mtu wa kutafakari mambo ya asili/vitu vya asili.

uhalisia wa mambo ya rohoni upo katika mambo ya asili. Ikiwa utakua mtu wa kutafakari kuna mambo mengi sana utaelewa na ndio maana sehemu nyingi sana Bwana Yesu alikua anatumia mifano ya kawaida kama ya mpanzi,mwivi,kupanda,kuvuna,wanawali,mfanya biashara nk ili kuelezea uhalisia uliopo hivyo watu wengi kuwa tunaichukulia kuwa kama mifano tu Yesu alikua anaongea tu lakini sio hivyo kabisa.

Marko 4:11-13 kawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu, bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa mifano,

[12] ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa.

[13 ] Akawaambia, Hamjui mfano huu? Basi mifano yote mtaitambuaje?

Unana hapo Bwana anawaambia kwa walio nje hufanywa kwa mifano kwa nini kwa mifano? Siku zote mifano huwa inaelezea uhalisia au mfano wa kitu halisi sasa mtu akishindwa kuelewa mfano wa hicho kitu halisi ukweli ni kwamba hataweza kuelewa kitu halisi. Ndio maana hata mashuleni ikiwa ni hesabu au fizikia au kemia nk kuna mifano mingi ambayo wanafunzi wanafundhishwa kwa lengo la kuwapa uelewa wa maswali watakayokutana nayo maana yake wakishindwa kuelewa hiyo mifano hawataweza kufanya maswali kama yakitoka.

vivyo hivyo ukitafakari ukuaji wa mmea,wanyama nk utajifunza jambo huenda unataka ukuaji wa kiroho na unataka uonekane kwako ndani ya wiki moja haiwezekani rudi kwenye asili itakufundisha na utajikuta unakua mvumilivu ukijua hufanyi kazi bure.

2.Omba ufunuo wa Roho Mtakatifu.

Hakuna imani pasipo ufunuo ufunuo ndio unaokupa wewe Imani ya kuendelea kusimama huwezi ukasema na Imani kabisa Mungu atatenda kitu ikiwa hakuna ufunuo watu tunaendelea mbele na kuwa na ujasiri kwa sababu ya ufunuo ambao Kristo anaachilia ndani yetu. Ukikosa ufunuo huwezi kuendelea wala usione ni kazi kupata ufunuo sio kazi kaa katika mazingira ya uwepo wa Mungu sio kanisani tu sehemu yeyote ukiwa mtu wa kutafakari kuna ufunuo utaupata.

Katika kutafakari kwangu siku moja nilipata ufunuo kwamba kila wazo lolote baya linalokuja katika ufahamu wangu, ikiwa ni kushindwa,nk nilikua Napata shida mwanzoni lakini baada ya kutafakari nikaelewa kila wazo negative ni uongo wala sio ukweli, ukweli uko kwenye biblia wazo likija la kushindwa kukata tamaa najua ni uongo unaojaribu kunitoa katika kweli ya neno ambalo linasema ninashinda na Zaidi ya kushinda wala hakuna chochote kinachiweza kunidhuru sawa sawa na Luka 10:19

3.Tunza ufunuo/weka kwenye ufahamu wako ufunuo huo.

watu wengi wanapata ufunuo juu ya kitu Fulani(maana nyingine ya ufunuo ni ukweli wa jambo) na shetani anapambana ili wewe usiujue ukweli wa jambo ili uendelee kutaabika kwa kitu kinachoitwa ujinga. Leo mtu anaweza kafahamu kitu Fulani kesho akaanza kusumbuka na kile kile kitu alichokipatia ukweli wake maana yake shetani kaiba na hutakiwi kumruhusu.

4.Soma neno,omba,soma vitabu vya watumishi wa Mungu,sikiliza mafundisho.

fanya haya yote ukiwa na ufahamu wa kuongezeka kukua usisikilize tu ili mradi basi kwa sababu hutaki kusikia vitu vya kidunia la! Kila unaposikiliza,unaposoma weka ufahamu wako na nia yako katika kupiga hatua na hivi ni vitu vitakavyokusaidia wewe kukua na kuongezeka usiwe mvivu wa kusoma kila siku hata kurasa tatu za kitabu kimoja au biblia tafakari unaweza kupitisha siku ngapo bila kusoma biblia,kitabu au kusikiliza mahubiri? Anza kupiga hatua. Unahitaji kujifunza kutoka kwa watumishi wengi ambao tayari wameshapitia hatua nyingi na kushinda.

Yapo meengi sana, lakini fanyia kazi haya machache mengine Bwana Yesu atakuongezea.

ubarikiwe sana.
@Nuru ya upendo
Mawasiliano:0613079530.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *