Tusome…
Mwanzo 37:6 “akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota.
7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake”.
Walawi 23: 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu;
11 naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa.
12 Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.
Neno mganda maana yake ni matita ya mazao ambayo yameshavunwa na kufungwa pamoja. Mfano: watu walipokuwa wakivuna ngano mashambani walizifunga katika matita matita na kuziweka pamoja halafu wakaenda kuzikoboa na kuzisaga. Matita hayo ndiyo hujulikana kama miganda.
Tuangalie kifungu hiki ili tuelewe zaidi
Kumbukumbu 24: 19 Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.
Hii ilimaanisha hivi, mtu akienda shambani kuvuna na akakusanya miganda kumi lakini wakati anaondoka akasahau mganda mmoja hakuruhusiwa kuurudia alitakiwa kuuacha kwa ajili ya mayatima na wageni, masikini walipewa ruhusa ya kuingia mashambani kuchukua masalia.
Jambo hili linatufundisha nini?
Kuna wakati Mungu hatakuruhusu uchukue kila kitu unachoona ni chako, ikitokea umesahau kumbuka kuwa ni mpango wa Mungu ili na wengine wapate kupitia wewe, usiwe mtu wa kumaliza vyote kuna wakati utakosa baraka zako. Ukisafiri usichukue nguo zote, unapoenda mahali na umebeba vitu vingi na ikatokea ukasahau kimojawapo basi endelea na safari maana huwezi kujua kwa nini Mungu ameruhusu ukisahau.
Wewe ni boss na kuna chenji zimabaki haina ulazima wa kuzichukua unaweza kuwaachia waajiriwa wako ili upate baraka.
Jambo lingine la kujifunza ni kutegemea Mungu zaidi ya miganda yetu. Yesu alifanya miujiza ya mikate akawambia mitume wakusanye vipande vyote bila kusahau hata kimoja, lakini wapoondoka eneo lile waligundua wamesahau mikate wakabishana wakijiuliza watakula nini. Yesu akawauliza mmesahau miujiza kama hiyo ambayo mmeshafanyiwa? Kwa nini kuwa na wasiwasi? Mungu atawapatia vingine hata kama mmesahau mlivyokuwa navyo.
Mathayo 16:5 Nao wanafunzi wakaenda hata ng’ambo, wakasahau kuchukua mikate.6 Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.
7 Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.
8 Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate?
9 Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota
Hivyo basi tujifunze tusiwe tunachukua miganda yote tusipishane na baraka..
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.